• HABARI MPYA

    Tuesday, October 16, 2012

    LIGI DARAJA LA KWANZA YAANZA OKTOBA 24, MAJIMAJI, ASHANTI ZARUDI KIVINGINE


    Na Princess Asia
    LIGI Daraja la Kwanza Tanzania Bara inatarajiwa kuanza rasmi Oktoba 24, mwaka huu kwa timu 18 kati ya 24 kujitupa kwenye viwanja tisa tofauti katika ligi hiyo inayochezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
    Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba Mechi za raundi ya kwanza za kundi A zitakazochezwa Oktoba 24 mwaka huu ni Burkina Faso dhidi ya Mbeya City (Jamhuri, Morogoro), Mlale JKT na Small Kids (Majimaji, Songea) na Kurugenzi Mufindi dhidi ya Majimaji (Uwanja wa Wambi, Mufindi mkoani Iringa).
    Amesema Mkamba Rangers na Polisi Iringa zitakamilisha raundi ya kwanza kwa kundi hilo Oktoba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, wakati mechi za raundi ya pili kwa kundi hilo zitachezwa Oktoba 27 mwaka huu kwa Polisi Iringa vs Mbeya City (Samora, Iringa), Majimaji vs Small Kids (Majimaji, Songea), Burkina Faso vs Mkamba Rangers (Jamhuri, Morogoro) na Kurugenzi Mufindi vs Mlale JKT (Wambi, Mufindi).
    Amesema raundi ya tatu ni Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Mbeya City vs Mlale JKT (Sokoine, Mbeya), Small Kids vs Mkamba Rangers (Nelson Mandela, Sumbawanga), Majimaji vs Burkina Faso (Majimaji, Songea) na Polisi Iringa vs Kurugenzi Mufindi (Samora, Iringa).
    Amezitaja timu za Kundi B ambazo zitamenyana Oktoba 24, mwaka huu ni Ndanda vs Transit Camp (Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara), Villa Squad vs Moro United (Mabatini, Pwani) wakati Oktoba 25 mwaka huu ni Green Warriors vs Tessema (Mabatini, Pwani) na Polisi Dar es Salaam vs Ashanti United (Chamazi, Dar es Salaam).
    Amesema raundi ya pili kwa kundi hilo ni Oktoba 27, mwaka huu Ndanda vs Green Warriors (Nangwanda Sijaona, Mtwara), Villa Squad vs Tessema (Mabatini, Pwani) wakati Oktoba 28 mwaka huu ni Ashanti United vs Transit Camp (Mabatini, Pwani) na Oktoba 29 mwaka huu ni Moro United vs Polisi Dar es Salaam (Chamazi, Dar es Salaam).
    Amesema Novemba 1, mwaka huu Green Warriors itamenyana na Ashanti United (Mabatini, Pwani), Novemba 2 mwaka huu ni Polisi Dar es Salaam vs Villa Squad (Chamazi, Dar es Salaam), Novemba 4 mwaka huu ni Tessema vs Ndanda (Chamazi, Dar es Salaam) na Transit Camp vs Moro United (Mabatini, Pwani).
    Amesema Kundi C nalo ambalo mechi zake zitachezwa Oktoba 24, mwaka huu ni kati ya Kanembwa FC vs Polisi Dodoma (Lake Tanganyika, Kigoma), Mwadui vs Morani (Kambarage, Shinyanga), Pamba vs Polisi Mara (Kirumba, Mwanza) na Rhino Rangers vs Polisi Tabora (Ali Hassan Mwinyi, Tabora).
    Amesema Raundi ya pili ni Oktoba 27 mwaka huu; Polisi Tabora vs Polisi Dodoma (Ali Hassan Mwinyi, Tabora), Mwadui vs Polisi Mara (Kambarage, Shinyanga), Kanembwa FC vs Morani (Lake Tanganyika, Kigoma) na Pamba vs Rhino Rangers (Kirumba, Mwanza), wakati Oktoba 31 mwaka huu ni raundi ya tatu; Polisi Mara vs Rhino Rangers (Karume, Musoma), Morani vs Polisi Tabora (Kiteto, Manyara), Polisi Dodoma vs Pamba (Jamhuri, Dodoma) na Kanembwa FC vs Mwadui (Lake Tanganyika, Kigoma).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: LIGI DARAJA LA KWANZA YAANZA OKTOBA 24, MAJIMAJI, ASHANTI ZARUDI KIVINGINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top