• HABARI MPYA

    Monday, June 04, 2012

    AMRI KIEMBA, SHAMTE WAREJEA SIMBA


    Haruna Shamte kushoto na Juma Kaseja enzi zake Simba SC 

    BEKI Ramadhani Haruna Shamte na kiungo Amri Ramadhani Kiemba wamemaliza muda wao wa kucheza kwa mkopo na wamerejea kwenye klabu yao, Simba SC ya Dar es Salaam.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Simba SC, Ibrahim Masoud ‘Maestro’ amesema leo mchana kwamba, Kiemba alikataa kabisa kwenda kuichezea Polisi Dodoma kwa sababu hawakufikia makubaliano, wakati Shamte aliichezea Villa Squad iliyoshuka daraja.
    Maestro ameiambia BIN ZUBEIRY mchana huu kwamba baada ya wachezaji hao kumaliza muda wao wa kuwa nje kwa mkopo, klabu itaangalia kama itawatoa tena kwa mkopo au itawarejesha kikosini.
    Lakini habari za ndani ambazo BIN ZUBEIRY imezipata ni kwamba wachezaji wote hao watarejeshwa kikosini, kwa sababu ya umuhimu wao na badala yake, beki Victor Costa na kiungo Salum Machaku ndio watatolewa kwa mkopo.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AMRI KIEMBA, SHAMTE WAREJEA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top