Manji |
YUSSUF Mehboob Manji, leo ametinga makao makuu ya Yanga,
makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani na kuwachukulia fomu za kugombea uongozi,
wanachama watatu, katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Julai 15, mwaka huu
mjini Dar es Salaam.
Kwa kitendo hicho cha kuingia Jangwani na kuchukua fomu,
wengi wamedhani Manji amechukua fomu za kugombea mwenyewe na tetesi zimeenea
Dar es Salaam kwamba anagombea Uenyekiti.
Lakini Katibu Mkuu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Francis
Kaswahili ameiambia BIN ZUBEIRY jioni hii kwamba Manji amewachukulia fomu wanachama
watatu, ambao ni Abdallah Bin Kleb na Muhingo Rweyemamu kwa ajili ya nafasi za Ujumbe
wa Kamati ya Utendaji na Isaac Chanji kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti.
Lakini bado kuna uvumi kwamba Manji mwenyewe wakati wowote
atachukua fomu ya kuwania Uenyekiti, ingawa awali ilielezwa anamuunga mkono Francis
Kifukwe awanie nafasi hiyo.
Kuchukua fomu kwa wajumbe hao watatu, kunafanya idadi ya
waliochukua fomu hadi sasa kufika 10, baada ya awali Ayoub Nyenzi kuchukua fomu
ya kugombea Makamu Mwenyekiti, Jumanne Mwamenywa, John Jambele, Peter Haule,
Gaudicius Ishengoma, Abdallah Sharia na Saleh Abdallah, wote
Ujumbe.
0 comments:
Post a Comment