![]() |
Ameota mbawa Jangwani; Uhuru Suleiman ameongeza mkataba Simba |
KIUNGO hodari, Uhuru Suleiman Mwambungu, au Robinho amesaini
mkataba mpya wa miaka miwili na klabu yake, Simba SC na hivyo kuzima ndoto za
Yanga waliokuwa wanamtaka mchezaji huyo kumpata.
Uhuru, aliyetua Simba misimu miwili iliyopita akitokea Mtibwa
Sugar ya Morogoro, iliyomtoa Coastal Union ya Tanga, ameiambia BIN
ZUBEIRY leo jioni kwamba ameongeza mkataba wa miaka miwili na klabu
yake.
“Kaka nimesaini mkataba mpya wa miaka miwili na hivi ninavyozungumza
na wewe nimekuja kwetu Mbeya kijijini kabisa kuchukua baraka za wazee, kisha nirudi
kazini na nguvu mpya,”alisema Uhuru.
Uhuru hakutaka kuwazungumzia Yanga, kwa sababu amesema
hakuwahi hata kukaa nao meza moja zaidi ya kusikia tetesi kwamba wanamtaka.
“Nilisikia Yanga walikuwa wananitaka, ila kwa kweli mimi
naona wamechelewa, kwa sababu nimekwishaongeza mkataba na timu yangu,”alisema.
Wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza Simba msimu huu, ambao
mikataba yao imeisha ni mabeki Juma Nyosso na Juma Jabu, ambao nao wanahusishwa
na mpango wa kuhamia kwa mahasimu wa jadi, Yanga.
0 comments:
Post a Comment