![]() |
Abdallah Bin Kleb |
ABDALLAH Ahmed Bin Kleb, amesema kwamba ameombwa na
wanachama wa klabu hiyo nchi nzima agombee nafasi ya Makamu Mwenyekiti, lakini
amewaomba kwa sasa aanzie kwenye Ujumbe, ili kukusanya uzoefu zaidi, kwani kwa
sasa anaamini bado hajapata uzoefu wa kutosha.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY usiku huu katika
mahojiano maalum, Bin Kleb alisema kwamba baada ya makubaliano hayo
wakapendekeza mtu mwingine wa kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti, wakati yeye
anagombea Ujumbe.
Bin Kleb alisema kwamba leo alikuwa kwenye msiba wa baba mkwe
wake Davis Mosha na akapigiwa simu na Yussuf Manji akimtaarifu kumchukulia fomu
ya kugombea Ujumbe wa Kamati ya Utendaji.
Bin Kleb alisema Manji naye ana mpango wa kuchukua fomu ya
kugombea Uenyekiti na na amepanga kufanya mambo makubwa mno katika Yanga,
ikiwemo kujenga Uwanja wa kisasa na kuwekeza fedha nyingi katika klabu, ili iwe
tishio kama Tout Puissant Mazembe iliyo chini ya milionea Moise Katumbi.
“Mimi binafsi namuunga mkono Manji na ninaomba wana Yanga
wote wamuunge mkono, kwa sababu ana mipango mizuri mno katika klabu,”alisema
Bin Kleb, ambaye ameridhia kugombea Ujumbe baada ya kuchukuliwa fomu na Manji.
Ingawa Katibu Mkuu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Francis
Kaswahili ameiambia BIN ZUBEIRY jioni hii kwamba Manji amewachukulia fomu Bin Kleb,
Muhingo Rweyemamu kwa nafasi ya Ujumbe na Isaac Chanji kwa nafasi ya Makamu
Mwenyekiti, lakini mtu mmoja aliye ‘beneti’ na milionea huyo mwenye asili ya
Kiasia, amesema Yussuf amechukua fomu leo ya kugombea Uenyekiti.
Kama Manji naye amechukua fomu, idadi ya waliochukua fomu
hadi sasa inafika watu 11, baada ya awali Ayoub Nyenzi kuchukua fomu ya
kugombea Makamu Mwenyekiti, Jumanne Mwamenywa, John Jambele, Peter Haule, Gaudicius
Ishengoma, Abdallah Sharia na Saleh Abdallah, wote Ujumbe.
Uchaguzi wa Yanga unaokuja baada ya Wajumbe wengi wa Kamati
ya Utendaji iliyoingia madarakani mwaka juzi, kujiuzulu akiwemo Mwenyekiti, Wakili
Lloyd Baharagu Nchunga unatarajiwa kufanyika Julai 15, mwaka huu na mwisho wa
zoezi la kuchukua ni keshokutwa
0 comments:
Post a Comment