![]() |
Banza akiimba na Twanga Pepeta, Leaders Club, Jumapili |
MWANAMUZIKI Ramadhani Masanja ‘Banza Stone’, kesho
anatarajiwa kutambulishwa katika bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ katika
onyesho la Usiku wa Mwafrika, kwenye ukumbi wa Club Billicanas, Dar es Salaam.
Habari zilizofikia BIN ZUBEIRY kutoka ndani ya uongozi
wa Twanga Pepeta, zimesema kwamba Banza amekwishamalizana na uongozi na kesho
atatambulishwa rasmi Billicanas.
Banza ambaye amekuwa akiimbia bendi ya Extra Bongo, alipanda
jukwaa la Twanga Pepeta kwa mara ya kwanza Jumamosi kwenye ukumbi wa Mango
Garden, Kinondoni, Dar es Salaam wakati Extra Bongo ikitumbuiza ukumbi wa
Meeda, Sinza.
Banza Jumapili
alipanda tena kwenye viwanja vya Leaders, Kinondoni na baada ya hapo akaingia
kwenye mazungumzo na uongozi wa bendi hiyo na imeelezwa wamefikia makubaliano
na Jenerali Mwana wa Masanja anarejea rasmi katika bendi iliyomuibua kimuziki,
mwaka 1998.
0 comments:
Post a Comment