Kagawa
KLABU ya Manchester United, hatimaye imemsajili kiungo wa Borussia
Dortmund, Shinji Kagawa kwa dau ambalo halijawekwa wazi na sasa kilichobaki ni mchezaji
huyo kufanyiwa vipo na kupewa kibali cha kufanya kazi Uinegereza, mambo ambayo
haina shaka yatakwenda sawa kwa nyota huyo aliyeichezea Japan mechi 30.
Tangu ajiunge na Dortmund kwa dau la pauni 285,000 akitokea Cerezo
Osaka mwaka 2010, Kagawa ameisaidia Dortmund kutwaa mataji mawili mfululizo ya Bundesliga,
akifunga mabao 29 katika mechi 71.
Kagawa alikuwa majeruhi wakati wa Kombe la Mataifa ya Asia
mwaka jana, ambayo yalimuweka nje ya Uwanja katika mzunguko wa pili wa msimu
wake wa kwanza Ujerumani.
Pamoja na hayo, nyota huyo wa Japan, alifungia mabao manane
katika mechi 18 katika msimu huo wa ligi na akatajwa kwenye kikosi cha msimu
cha Bundesliga.
Msimu huu, ameiwezesha pia Dortmund kutwaa taji la DFB-Pokal
kwa mara ya tatu katika historia ya klabu hiyo.
Lakini kukosekana kwenye kikosi cha Japan katika Fainali za
Kombe la Dunia mwaka 2010, kuna uwezekano Manchester United italazimika kukata
rufaa ili apatiwe kibali cha kufanya kazi Uingereza.
Kwa sasa, Kagawa anakosa vigezo vya moja kwa moja vya England,
kuwa ameitumikia timu yake ya taifa kwa asilimia 75 katika miaka miwili
iliyopita, aingawa hadhi yake kuwa mshindi wa mataji mawili ya Bundesliga itamfungulia
milango ya kukipiga Old Trafford.
0 comments:
Post a Comment