Mosimane
KOCHA Pitso Mosimane amepoteza kazi katika timu ya taifa ya
soka ya Afrika Kusini, baada ya kufukuzwa rasmi mchan wa leo.
Mosimane aliondoka mara moja katika kambi ya timu, hoteli ya
Royal Marang mjini Phokeng, Rustenburg baada ya kufukuzwa kwake kuthibitishwa
na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika Kusini (SAFA), Robin
Peterson.
Bafana Bafana imeshindwa imeshindwa kushinda hata mechi moja
katika mechi saba, ikiwemo ya sare ya 1-1 na Ethiopia Jumapili.
Nahodha wa zamani, Steve Komphela, ambaye aliteuliwa kuwa
Msaidizi wa Mosimane, mapema Aprili, sasa atakuwa kocha wa muda wa timu hiyo.
Komphela ataiongoza Bafana katika mechi ya kuwania tiketi ya
kucheza Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil dhidi ya Botswana Jumapili, Juni
9 mjini Gaborone na mchezo wa kirafiki dhidi ya Gabon, Juni 15.
SAFA imeripotiwa kuandaa ofa kwa kocha wa Moroka Swallows,
Gordon Igesund, ambaye kwa sasa yupo China na Dube Birds, lakini inasemekana
hivi sasa yuko njiani kurejea nchini humo kujadili dili hilo la kuinoa timu ya
taifa..
0 comments:
Post a Comment