Published: 29 minutes ago
JERMAIN DEFOE amerejea kwenye kambi ya timu ya taifa ya England asubuhi ya leo akitoka kwenye mazishi ya baba yake mzazi.
Mshambuliaji huyo wa Tottenham, alirejea nyumbani Alhamisi asubuhi baada ya kupata habari hizo za kuhuzunisha.
Pamoja na hayo amejiunga tena na wenzake kambini majira ya saa 3 asubuhi na alitarajiwa kushiriki mazoezi katika Uwanja ambao mashabiki hawataruhusiwa kuingia.
England inajiandaa kwa mechi ya ufunguzi ya Kundi D Jumatatu dhidi ya Ufaransa mjini Donetsk.
Kocha Roy Hodgson anafurahia kurejea kjwa Defoe kikosini.
Pamoja na hayo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, hatarajiwi kuanza Jumatatu dhidi ya Ufaransa.
Ashley Young anatarajiwa kuchukua nafasi ya ushambuliaji, katika mechi hiyo badala ya Wayne Rooney anayetumikia adhabu.
Andy Carroll na Danny Welbeck wanatarajiwa kuwa washambuliaji wengine pamoja na mshambuliaji huyo wa Manchester United.
Carroll alicheza pamoja na Young katika mazoezi ya wazi jana.
Pamoja na hayo, mshambuliaji huyo wa Liverpool alikuwa mmoja wa waliotembelea Auschwitz na FA jana.
0 comments:
Post a Comment