Getty
LIGI Kuu ya England itawakilishwa vizuri katika michuano ya
Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2012 kwa asilimia 20 ya wachezaji wanaokwenda kwenye
michuano hiyo kutoka kwenye klabu za Ligi hiyo ambao waling’ara msimu wa 2011-12.
Uchambuzi uliofanywa na shirika la Sports Business Group
huko Deloitte, umegundua asilimia 74 ya wachezaji wote 368 wa vikosi 16 vitakavyosafiri
kwenda kwenye fainali hizo zinazoandaliwa kwa pamoja na Poland na Ukraine wanatoka
ligi nyingine.
Bundesliga ya Ujerumani ni ligi nyingine inayofuatia, ikiwa
na asilimia 13 ya wachezaji kwenye michuano hiyo, ikifuatiwa na Hispania, La
Liga yenye asilimia 9, Italia, Serie A na Urusi, Liga zote zikiwa na asilimia 9.
Wakati wachezaji wengine watano zaidi wakicheza Ligi Daraja
la Kwanza England, Championship msimu wa 2011-12, England pia ni taifa pekee,
ambalo wachezaji wake wote 23 wanacheza ligi ya nchini mwao.
Dan Jones, ofisa wa shirika hilo amesema: “Uwakilishi wa nguvu
kutoka Ligi Kuu ya England katika Euro 2012 ni matokeo ya kuwa na ligi nzuri,
inayohusisha wachezaji bora kutoka nchi tofauti duniani.
Amesema pia wamegundua mapato ya Ligi Kuu yameongezeka kwa
asilimia 12 hadi kufika pauni Bilioni 2.3 msimu wa 2010-11.
Ongezeko la mapato hayo yanatokana na vyanzo vya kibiashara,
huku ongezeko la asilimia 18 likipatikana hadi pauni Milioni 600, lakini pato
kubwa zaidi kwa klabu za England linatokana na mapato ya matangazo, ambalo ni
pauni Bilioni 1.18, huku Ligi Kuu ikiwapiku wapinzani wanaowakaribia, Bundesliga,
kwa asilimia 40 ya mapato.
0 comments:
Post a Comment