![]() |
Gerd Muller wa sasa |
Katika kitabu chake kiitwacho Brilliant Orange: The Neurotic
Genius of Dutch Football, David Winner anaandika; Muller alikuwa mfupi, hana
sura ya mvuto na hana kasi; hakuwa mchezaji
unayeweza kusema ni mkali, lakini alikuwa mzuri katika mipira ya juu na
uchu wa kufunga mabao. Miguu yake mifupi ilimwezesha kugeuka haraka na kukimbia
kiasi cha kufanya wachezaji wa timu pinzani kuanguka wanapomkimbiza. Aidha
alikuwa na uwezo wa kufunga katika mazingira magumu.
Huyo ni Gerhard ‘Gerd’ Müller aliyezaliwa Novemba 3, mwaka 1945
mjini Nordlingen, ambaye alikuwa
mchezaji muhimu na mfungaji bora wa zamani nchini Ujerumani.
![]() |
Gerd Muller enzi zake |
Ufungaji bora wa Müller unajidhihirisha yenyewe. Amefunga
magoli 68 katika michezo 62 akiwa na timu ya taifa, mabao 365 katika michezo 427
ya Bundesliga (Ligi Kuu nchini Ujerumani) na rekodi ya mabao 66 ya kimataifa
katika michezo 74 ya Klabu Ulaya. Müller kwasasa anashikilia nafasi ya nane kwa
ufungaji bora katika mechi za kimataifa licha ya kucheza michezo michache
ukilinganisha na wachezaji wengine katika orodha ya wachezaji 15 bora. Majina
yake ya utani ni “Bomber der Nation” (Mlipuaji mzuri kuongoza taifa) na
“kleines dickes Müller” (Mfupi mnene Müller, uongo wa mkubwa).
Mwaka wa 1970, Müller alichaguliwa Mchezaji Bora wa Mwaka
Ulaya baada ya mafanikio msimu huo akiwa na Bayern Munich ambapo alifunga mabao 10 katika Kombe
la Dunia 1970 FIFA. Kabla ya bao ambalo alifunga Ronaldo katika mechi dhidi ya Ghana hatua
ya 16 Bora Kombe la Dunia 2006, Müller alikuwa anashikilia ufungaji bora wa
mashindano hayo kwa mabao 14, rekodi iliyodumu kwa miaka 32.
Alianza kucheza soka katika klabu ya TSV 1861 Nördlingen.
Müller alijiunga na FC Bayern Munich
mwaka 1964 ambapo aliungana na wachezaji nyota wa baadaye Franz Beckenbauer na
Sepp Maier. Klabu hii (Bayern Munich) aliyokuwa anaichezea Müller ilikuja ikawa
maarufu. Akiwa na Bayern Munich, Müller alishinda mataji mengi katika miaka ya
1960 na 1970: Alishinda Ubingwa wa Ujerumani mara nne, Ubingwa wa Ulaya mara
tatu, Ubingwa wa Mabara mara moja, na Ubingwa wa Mabingwa Ulaya mara moja. Uimara
wake wa kufunga mabao ulimfanya awe mfungaji bora nchini Ujerumani mara saba na
mfungaji bora Ulaya mara mbili. Müller anashikilia ufungaji bora ndani ya msimu
moja katika Bundesliga kwa rekodi ya mabao 40 katika msimu wa 1971–72.
Muller alifunga mabao 68 katika michezo 62 akiwa na timu ya
Ujerumani Magharibi. Alianza kuichezea timu ya taifa mwaka wa 1966 na kustaafu Julai
7, 1974 baada ya kushinda Kombe la Dunia lililoandaliwa katika uwanja wake wa
nyumbani jijini Munich .
Alifunga bao la ushindi katika mechi la fainali ambapo waliwafunga Uholanzi 2-1.
Mabao yake manne na yale 10 katika Kombe la Dunia 1970 lilimfanya awe mfungaji
bora katika michuano hiyo na jumla ya mabao 14; rekodi ambayo ilidumu hadi mwaka
2006 ambapo Ronaldo alimpiku. Cha kushangaza ni kwamba Kombe la Dunia 2006
ilifanyika nchini Ujerumani. Ronaldo, mshambuliaji wa Brazil , alifunga bao la 15 na kumpiku Müller katika
mechi dhidi ya Ghana
iliyochezwa Juni 27, 2006.
Baada ya kucheza Bundesliga, alienda Marekani ambapo
alijiunga na Fort Lauderdale Strikers mwaka ya 1979 inayoshiriki Ligi ya
Marekani Kaskazini. Alicheza misimu mitatu na timu hii akifunga mabao 38 na
nyakati moja kufika fainali lakini kupoteza mwaka 1980.
Baada ya Müller kustaafu soka mwaka 1982, alijikuta akiwa
mlevi wa kupindukia. Hata hivyo, wafariki zake katika timu ya Bayern Munich walimsihi
kwenda kupata ushauri nasaha. Na alipopata nafahu, alipewa kazi ya ukocha
katika timu ya Bayern Munich II ambapo anafanya kazi hadi leo. Pia kuna vifaa
vya michezo vinavyotolewa na kampuni ya Adidas chini ya jina la Gerd Müller. Ni
sehemu ya mzigo mpya ya adidas. Julai mwaka 2008, uwanja wa Rieser Sportpark
uliopo in Nördlingen ambapo Müller alianza kucheza soka ulibadilishwa jina na
kuitwa Gerd-Müller-Stadion kwa heshima ya mshambuliaji huyo.
WASIFU WAKE:
JINA: Gerhard Müller
KUZALIWA: Novemba 3, 1945
ALIPOZALIWA: Nordlingen, Ujerumani
KLABU ALIZOCHEZEA:
Mwaka Klabu
1963–1964 1861
Nördlingen (Mechi 32, mabao 51)
1964–1979 Bayern
Munich (Mechi 453, mabao 398)
1979–1981 Fort
Lauderdale Strikers (Mechi 80, mabao 40)
(Tangu 1966 hadi 1974, aliichezea Ujerumani Magharibi mechi
62, akaifungia mabao 68)
0 comments:
Post a Comment