![]() |
Ngassa 'aliua' Tembo 2009 |
Huu utakuwa mchezo wa pili kwa kocha mpya wa Tanzania, Kim
Poulsen baada ya sare ya bila kufungana na Malawi, Dar es Salaam na amejipanga
kukabiliana na timu hiyo tishio zaidi Afrika kwa sasa.
Kwa upande wa wenyeji, Sabri Lamouchi ni kocha mpya kabisa katika
kikosi cha Tembo, kufuatia kufukuzwa kwa Francois Zahoui wiki iliyopita.
Tanzania haijawahi kabisa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia
na ni miongoni mwa ndoto za Kim Poulsen anazotaka kutimiza akiwa kocha wa Taifa
Stars.
Kundi hilo C la kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe
la Dunia mwaka 2014 Brazil, linahusisha pia timu za Gambia na Morocco ukiondoa
Ivory Coast na Tanzania.
“Tunawaheshimu Ivory Coast kama timu ambayo inaundwa na
wachezaji nyota duniani, kama Didier Drogba na Yaya Toure, na ambao wanacheza
klabu kubwa Ulaya, lakini lazima wajiandae kupata wakati mgumu kutoka kwetu”, alisema
Poulsen baada ya mazoezi yake ya kwanza mjini Abidjan jana.
![]() |
Drogba aliifunga Stars 2010 |
Mechi za karibuni kuzikutanisha timu hizo, ilikuwa mwaka
2009, katika michuano ya CHAN, ambayo Tanzania iliwafunga wenyeji 1-0, beo
pekee Mrisho Ngassa wa Azam FC, enzi hizo akitokea Yanga na mwaka 2010, Ivory
Coast walilipa kisasi Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki, bao pekee la
Nahodha Didier Drogba.
Wachezaji walio kambini mjini Abidjan kwenye kikosi cha
Tembo Mkubwa ni makipa Ibrahim Kone na Badra Sandre, mabeki Kolo Toure,
Emmanuek Eboue, Benjamin Angoua, Steve Gohouri, Brice Dja Djedje na Guy Demel,
viungo Yaya Toure, Didier Zokora, Kafoumba Coulibaly, Marco Né, Moussa Kone,
Romaric na Emerse Faé na washambuliaji Didier Drogba (Nahodha), Salomon Kalou,
Serges Deble na Adama Bakayoko.
Kwa upande wa Tanzania, nyota walio na timu Abidjan ni makipa
Juma Kaseja (Nahodha), Mwadini Ally na Deogratius Munishi, mabeki Aggrey
Morris, Amir Maftah, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Waziri Salum, Shomari
Kapombe na Juma Nyoso, viungo Mwinyi Kazimoto, Salum Abubakar, Shaaban Nditi,
Edward Christopher, Mrisho Ngasa, Frank Domayo na washambuliaji Mbwana Samatta,
John Bocco, Simon Msuya na Ramadhan Singano ‘Messi’.
TAARIFA ZA MECHI:
KUANZA: Saa 3.00
usiku (Afrika Mashariki, 11 jioni Ivory Coast)
UWANJA: Stade Felix
Houphouet-Boigny (watu: 35,000).
REFA: Slim Jedidi
(Tunisia).
WASAIDIZI: Bechir
Hassani (Tunisia) na Sherif Hassan (Misri).
REFA WA AKIBA:
Youssef Essrayri (Tunisia).
MECHI NYINGINE ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA AFRIKA LEO | ||||
15:00 | Kenya | v | Malawi | Nairobi |
16:00 | Central African Republic | v | Botswana | Bangui |
16:30 | Cameroon | v | Congo DR | Yaounde |
18:30 | Sierra Leone | v | Cape Verde | Freetown |
18:30 | Gambia | v | Morocco | Bakau |
19:00 | Sudan | v | Zambia | Khartoum |
19:00 | Ivory Coast | v | Tanzania | Abidjan |
19:00 | Tunisia | v | Equatorial Guinea | Monastir |
20:00 | Burkina Faso | v | Congo | Ouagadougou |
20:00 | Senegal | v | Liberia | Dakar |
21:30 | Algeria | v | Rwanda | Blida |
MECHI NYINGINE ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA AMERIKA KUSINI | ||||
20:00 | Uruguay | v | Venezuela | Montevideo |
22:10 | Bolivia | v | Chile | La Paz |
0 comments:
Post a Comment