MMILIKI wa klabu Shanghai Shenhua, Zhu Junb alianza kwa pamoja na Nicolas Anelka katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo katika mechi ya kirafiki hivi karibuni .
Bilionea huyo wa Kichina, alicheza kwa dakika 45 kabla ya kutolewa mapumziko, Shenhua ikitoka sare ya 1-1 na CN Sports ya Argentina, katika mechi ambayo Anelka alikosa penalti kipindi cha pili.
Junb, mwenye umri wa miaka 45, alivaa jezi namba 11, lakini alipoteza nafasi kibao ambazo zinaweza kumshawishi kumletea Anelka pacha wake wa zamani, Drogba, ambaye kwa sasa yuko huru baada ya kubwaga manyanga Stamford Bridge.
Kocha mchezaji Nicolas Anelka kazini
Baada ya mechi hiyo, Zhu aliendelea kutoonyesha nia ya moja kwa moja ya kumchukua mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34, mwenye Medali ya Dhahabu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, akisema: 'Hilo ni swali zuri. Lakini siwezi kukujibu leo.’
Anelka alijiunga na Shenhua Januari, mwaka huu na lazima aombe sana ombi lake la kuletewa Drogba likubaliwe
Pia, Junb anafikiria kumsajili na Fernando Torres…
0 comments:
Post a Comment