Tetesi za J'mosi magazeti Ulaya
LAMBERT KUIBOMOA NORWICH
MARA alipothibitishwa tu kama kocha wa Aston Villa, Paul Lambert amepanga kurudi kwenye klabu yake ya awali, Norwich kumbeba Nahodha na mshambuliaji nyota, Grant Holt, mwenye umri wa miaka 31.
KLABU ya Paris St Germain sasa inaandaa dau la pauni Milioni 100 kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney, mwenye umri wa miaka 26, kwa mujibu wa vyanzo barani Ulaya. Awali vyanzo nchini Ufaransa vilisema PSG inamtaka Rooney kwa Euro Milioni 150.
KOCHA mpya wa Liverpool, Brendan Rodgers ameripotiwa kuwa tayari kumsajili kiungo wa Everton, Marouane Fellaini, mwenye umri wa miaka 24.
GWIJI wa soka Argentina, Diego Maradona ambaye kwa sasa ni kocha wa Al Wasl ya Dubai, amesema wana nia ya dhati kabisa ya kumsajili mshambuliaji mkongwe, aliyebwaga manyaga Chelsea, Didier Drogba mwenye umri wa miaka 34.
KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini amesema klabu yake itawasilisha ombi la kumsajili kwa pauni Milioni 25, mfungaji bora wa Ligi Kuu England, Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 28, iwapo Arsenal watashindwa kumshawishi Mholanzi huyo kusaini mkataba mpya.
KLABU ya Southampton imepanga kumsajili kwa dau la pauni Milioni 3, Jack Butland, kinda wa miaka 19 anayeidakia Birmingham, ambaye yumo kwenye kikosi cha England cha Euro 2012.
KLABU ya Real Socieded iko tayari kuvunja benki yake ili kumbeba moja kwa moja mshambuliaji wa Arsenal, Carlos Vela, mwenye umri wa miaka 23, baada ya kuvutiwa naye akiwa anawatumikia kwa mkopo msimu uliopita.
KLABU ya Inter Milan imeanza rasmi harakati za kuwania saini ya mchezaji anayetakiwa na Chelsea, Lucas Moura kutoka Sao Paulo kwa dau la pauni milioni 19 kwa ajili ya kinda hilo la miaka 19 - lakini ofa hiyo imepigwa chini.
KLABU za Chelsea na Manchester United zote zimeonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Fulham, Moussa Dembele, mwenye umri wa miaka 24, ana zimeanza mazungumzo kwa dau la pauni Milioni 10.
MANCINI: AGUERO ATAKUWA MESSI
KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini amesema mshambuliaji wake Sergio Aguero anaweza kuwa kama Lionel Messi na kupiga mabao katika kila mechi.
0 comments:
Post a Comment