IMEWEKWA OKTOBA 4, 2013 SAA 6:32 MCHANA
WACHEZAJI wa Manchester United waliamua kujifariji na mwanzo mbaya wa msimu wa timu yao kwa kuhudhuria onyesho la rapa Jay-Z jana.
Wilfried Zaha, Danny Welbeck, Ashley Young na Patrice Evra walipigwa picha wakitoka kwenye onyesho hilo.
Welbeck - akitoka kufunga bao katika Ligi ya Mabingwa dhidi ya Shakhtar Donetsk katikati ya wiki- alikuwa mwenye furaha na tofauti na wenzake watatu baada ya shoo hiyo ya Hip hop.
Furaha kama Ashley? Danny Welbeck akiwa mwenye tabasamu pana, wakati Ashley Young akiwa ameinamisha kichwa chini wakati wanaondoka
Niangalie! Shabiki mmoja mwenye furaha alipigwa picha karibu na Patrice Evra, wkati Wilfried Zaha akiondoka kinyonge
Mtu mzima ndani ya nyumba: Nyota wa United walikuwa Manchester kuangalia shoo ya Jay-Z
Kikosi cha David Moyes kitasafiri Sunderland kwa ajili ya mechi ya Jumamosi, kikiwa na matarajio ya kizunduka baada ya kufungwa mechi tatu kati ya nne za Ligi Kuu England.
Wako chini mno kwenye msimamo, nafasi ya 12 wakizidiwa pointi nane na vinara Arsenal na wazi wanahitaji pointi Uwanja wa Light kujiweka sawa.
Chini na juu: David Moyes amekuwa katika mwanzo mgumu ndani ya miezi yake miwili ya awali kama kocha wa United
Hoi: United ilifungwa nyumbani na West Brom ikitoka kufungwa na Manchester City wiki moja kabla
Lakini kufuatia sare ya Ukraine, bila shaka United wataingia na moto mkali dhidi ya Black Cats.
Wakati huo huo, Ryan Giggs amesema wachezaji ndio wanaostahili lawama kwa mwanzo mbaya na si Moyes.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 39- amejitolea kumtetea bosi wake, akisema: "Siwezi kumnyooshea mtu kidole kwa haya yanayotokea. Hatujacheza vizuri inayostahili wote kama wachezaji binafsi na hata kama timu,"alisema.
kazi nzuri: Welbeck aliifungia United bao la kusawazisha katikati ya wiki Ligi ya Mabingwa
"Tunafahamu ubora katika chumba cha kuvalia nguo. Sisi ni mabingwa, hivyo tulionyesha ubora mwaka jana na tunatakiwa kuonyesha tena,".
"Sir Alex alikuwa kocha babu kubwa na mwenye nguvu kubwa katika klabu. Utamkumbuka mtu kama huyo. Lakini sifikiri kwamba inaweza kuwa sababu wakati wachezaji hawachezi vizuri kibinafsi kama wanayotakiwa.
"Hatuchezi vizuri kama timu. Hatujapata tatizo la majeruhi kama tulilokuwa nalo kipindi kilichopita- hakuna kisingizio,"alisema.