• HABARI MPYA

    Sunday, June 08, 2014

    DIEGO COSTA AKIRI ANAKWENDA CHELSEA

    MSHAMBULIAJI wa Hispania, Diego Costa amepiga hatua nyingine katika kuthibitisha yuko karibu kuhamia Chelsea kwa dau la Pauni Milioni 32, baada ya jana kusema 'inaonekana hivyo' kufuatia kuulizwa kama atajiunga na kikosi cha Jose Mourinho.
    Akizungumza baada ya mechi ya kirafiki kujiandaa na Kombe la Dunia, ambayo Hispania iliifunga 2-0 El Salvador jana, Costa alisema: "Ninakwenda Chelsea? Inaonekana hivyo,".
    Costa alicheza kwa mara ya kwanza kikosini Hispania jana tangu aumie kwenye Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi uliopoita, klabu yake, Atletico Madrid ikifungwa 4-1 na wapinzani wao, Real ndani ya dakika 120 licha ya kuongoza 1-0 hadi dakika ya 90 na ushei.
    Mpachika mabao huyo mwenye umri wa miaka 25, alionekana yuko fiti kabisa ingawa alitolewa dakika ya 74 kumpisha Xavi Hernandes, lakini alicheza vizuri na alitoa mchango katika bao la kwanza dakika ya 60 lililofungwa na David Villa, ambaye pia alifunga na la pili.      
    Amekubali: Diego Costa ameweka wazi kuwa mbioni kuhamia Chelsea kwa dau la Pauni Milioni 32
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DIEGO COSTA AKIRI ANAKWENDA CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top