• HABARI MPYA

    Saturday, June 07, 2014

    KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2014; KUNDI F LENYE UTAMU WA MESSI, DI MARIA, WAKALI WENGINE KIBAO NA NIGERIA

    TIMU yenye mashabiki wengi, Argentina ipo kundi moja na Bosnia & Herzegovina, Iran na Nigeria katika Kombe la Dunia mwaka huu.
    BIN ZUBEIRY, inaendelea kukuletea makala za mchambuzi na beki wa zamani wa England, Martin Keown hapa akilichambua Kundi F.

    Wakali: Kikosi cha kwanza cha Argentina kabla ya kuifunga Trinidad and Tobago katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na Kombe la Dunia
    Kundi F
    Argentina
    Nigeria
    Iran
    Bosnia & Herzegovina
    Utabiri wa Keown;
    1 Argentina
    2 Nigeria
    3 Bosnia
    4 Iran
    Ratiba (Saa za Afrika Mashariki)
    Jun 15        Argentina v Bosnia  Saa 7:00 usiku R. Janeiro
    Jun 16       
     Iran v Nigeria           Saa 4:00 usiku  Curitiba
    Jun 21        
    Argentina v Iran       Saa 1:00 usiku B.Horizonte
    Jun 21        
    Nigeria v Bosnia      Saa 7:00 usiku Cuiaba
    Jun 25        
    Nigeria v Argentina  Saa 1:00 usiku Porto Alegre
    Jun 25        
    Bosnia v Iran           Saa 1:00 usiku Salvador
    ARGENTINA   
    Viwango vya FIFA: Namba 5
    Kocha: Alejandro Sabella. Akiwa mchezaji alipewa jina la utani ‘kocha polepole’ lakini hakuna pole pole katika timu yake.
    Nahodha: Lionel Messi (Barcelona)
    Mchezaji wa kumulikwa: Lionel Messi (Barcelona). Fainali za mwaka 1970 za Kombe la Dunia zilikuwa za Pele, Maradona akamiliki za 1986. Hatimaye huu unaweza kuwa mwaka wa Lionel Messi. Amemfunika Maradona kwa umaarufu, lakini hajafanya lolote la manna katika Fainali mbili zilizopita za Kombe la Dunia. Sasa, Argentina imepata nafasi ya kumuibua.
    Time to deliver: Argentina superstar Lionel Messi hasn't delivered on the biggest stage of all... yet
    Wakati wa kufanya kweli: Nyota wa Argentina, Lionel Messi hajafanya makubwa bado kwenye Kombe la Dunia

    Ubora wao: Wanashambulia, Argentina wana vipaji vingi vya washambuliaji, lakini lazima wavitumie vizuri. Messi anaonekana kucheza vizuri akiwa amezungukwa na Sergio Aguero na Gonzalo Higuain pembeni yake.
    Tatizo: Kupata uwiano sahihi. Wanaweza kuwa hatari wanaposhambulia, lakini wakishambuliwa wao wanapitika na kufungwa kutokana na safu yao ya ulinzi kukosa mabeki wa kiwango cha dunia.
    Watakwenda England? Marcos Rojo wa Sporting Lisbon alikuwa kwenye mipango ya Liverpool, Chelsea inamtaka Ezequiel Lavezzi na Angel di Maria anatakiwa na Arsenal, City na Chelsea. Kiungo wa Benfica, Enzo Perez anatakiwa na Man United.
    Matokeo mazuri kombe la Dunia: Washindi (1978 na 1986)
    Walivyofika hapa: Waliongoza kundi la Amerika Kusini katika mechi za kufuzu, wakiizidi kwa pointi mbili Colombia wakifungwa mechi mbili tu kati ya 16.
    Je, wajua? Kocha Sabella ni mwenyeji Yorkshire. kati ya mwaka 1978 na 1981 alichezea kwa misimu miwili Sheffield United na mwaka mmoja Leeds.
    BOSNIA & HERZEGOVINA    
    Viwango vya FIFA: Namba 21
    Kocha: Safet Susic. Mchezaji mzuri pia enzi zake, Susic aliifungia hat-trick Yugoslavia dhidi ya Argentina mwaka 1979.
    Nahodha: Emir Spahic (Bayer Leverkusen)
    Mchezaji wa kumulikwa: Miralem Pjanic (Roma). Edin Dzeko anafunga mabao, lakini Pjanic anayetengeneza. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anafanya kazi nzuri sana katika nafasi ya kiungo, ni hodari wa kutoa pasi za mwisho.
    Goal machine: Edin Dzeko, the Manchester City striker, is the main threat for Bosnia and Herzegovina
    Mtambo wa mabao: Edin Dzeko, mshambuliaji wa Manchester City, ni tegemeo la Bosnia and Herzegovina

    Ubora wao: Kufunga mabao. Walifunga mabao 30 wakati wa kampeni za kufuzu, shukrani kwa mfumo wao unaolipa wa 4-4-2 ya kushambulia moja kwa moja.
    Hatari: Wanacheza kawaida. Kwa mfumo wanaotumia, wanaweza kudhibitiwa kwa urahisi.
    Watakwenda England? Vedad Ibisevic wa Stuttgart ni mshambuliaji pacha wa Dzeko ambaye amezivutiwa Aston Villa na Stoke. Pjanic pia anavutia Ligi Kuu ya England, lakini Roma hawawezi kumuuza.
    Matokeo mazuri Kombe la Dunia: 2014 wanashiriki kwa mara ya kwanza
    Walivyofika hapa: Walimaliza pointi saws na Ugiriki katika kundi lao, lakini wakafuzu katakana na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
    Je, wajua? Mwaka 2004 kocha Susic alishinda tuzo ya mchezaji bora wa nchi yake– mchezaji bora kwa miaka 50 iliyopita na mwaka 2012 alishinda tuzo ya mchezaji bora wa kigeni katika Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1.
    IRAN       
    Viwango vya FIFA: Namba 43
    Kocha: Carlos Queiroz. Iran ni nchi ya nne kocha Queiroz anaiongoza baada ya Ureno, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Afrika Kusini.
    Nahodha: Javad Nekounam (Al-Kuwait)
    Mchezaji wa kumulikwa: Reza Ghoochannejhad (Charlton) Akiwa anafahamika kwa wachezaji wenzake kwa nina la utani ‘Gucci’, mshambuliaji huyo ana mguu 'mtamu' wa kushoto na amefunga mabao fulani muhimu Iran. Alikuwa mfungaji wao bora katika mechi za kufuzu.
    The boss: Experienced Carlos Queiroz is the man in charge of Iran's World Cup campaign
    Bwana mkubwa: Kocha mzoefu Carlos Queiroz ataiongoza Iran Kombe la Dunia mwaka huu

    Ubora wao: Wanacheza kwa utulivu. Queiroz ni muumini wa nidhamu mchezoni na anapenda timu yake kuzama ndani, lakini wanaposhambuliwa na wapinzani, Iran wanaweka kambi kwenye eneo lao hadi wapokonye mpira.
    Hatari: Kumudu kupambana na vigogo. Wanafanya vizuri katika mechi za kufuzu bars la Asia, lakini wanasota kufanya vizuri dhidi ya timu za kiwango cha ubora wa dunia.
    Watakwenda England? Mtu mmoja wa kummulika ni kiungo Alireza Jahanbakhsh wa NEC ambaye amekuwa akihusishwa na kuhamia Manchester United. Ashkan Dejagah wa Fulham anaweza kurudi Ligi Kuu England.
    Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Hatua ya makundi (1978, 1998 na 2006)
    Walivyofika hapa: Hawakufungwa katika hatua ya kwanza ya kufuzu kwenye kundi lao Asia, kabla ya kuongoza Kundi A mbele ya Korea Kusini. 
    Je, wajua? Likiwa na herufi 14, Ghoochannejhad ndilo nina urefu zaidi la ukoo katika soka ya Engand.
    NIGERIA   
    Viwango vya FIFA: Namba 44
    Kocha: Stephen Keshi. Alistaafu siku moja baada ya kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013, lakini akabadili uamuzi wake ndani ya saa 24.
    Nahodha: Vincent Enyeama (Lille)
    Mchezaji wa kumulikwa: Kenneth Omeruo (Chelsea). Amekuwa akicheza kwa mkopo Uholanzi na Middlesbrough, lakini ana nafasi kubwa ya kuw abeki bora duniani baadaye. Anajituma na ana maarifa na ufundi pia- tarajia siku akikutana na Messi litakuwa bonge la picha.
    Good luck with that: Kenneth Omeruo will be trying to keep Messi under control when Nigeria play Argentina
    Kuwa naye bahati: Kenneth Omeruo anatarajiwa kumdhibiti Messi wakati Nigeria itakapocheza na Argentina

    Ubora wao: Wanajituma. Keshi anaiacha timu yake ishambulie na ndiyo maana mwaka 2013 walishinda Kombe la Mataifa ya Afrika. Beki zao za pembeni zinashambulia mwanzo mwisho.
    Hatari: Kumudu presha. Timu ya Keshi ni nzuri, lakini ni wachezaji wanne tu kikosini mwake wamecheza Kombe la Dunia kabla.
    Atakwenda England? Emmanuel Emenike amewahi kutakiwa na Tottenham hata Liverpool na Everton. Klabu yake, Fenerbahce inamthaminisha mshambuliaji huyo mwenye kasi kwa dau la Pauni Milioni 15.
    Matokeo mazuri Kombe la Dunia: 16 Bora (1994 na 1998)
    Walivyofika hapa: Hawakufungwa katika kundi lao kabla ya kuifunga Ethiopia mabao 4-1 katika mechi mbili za nyumbani na ugenini za mchujo wa mwisho kwa Afrika hivyo kujikatia tiketi ya Brazil.
    Je, wajua? Kocha Keshi ni kati ya watu wawili tu pamoja na Mahmoud El-Gohary wa Misri, kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika kama mchezaji na kocha.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2014; KUNDI F LENYE UTAMU WA MESSI, DI MARIA, WAKALI WENGINE KIBAO NA NIGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top