Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
KOCHA Mart Nooij amewaanzisha pamoja washambuliaji Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, Mrisho Ngassa na John Bocco katika mchezo wa kwanza dhidi ya Msumbiji, hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco.
Katika mchezo huo, utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo, Mholanzi huyo amewaanzisha pia viungo Mwinyi Kazimoto katika dimba la chini na Erasto Nyoni juu yake.
Ngassa na Ulimwengu watashambulia pembeni wakati Bocco na Samatta watacheza mbele ya mdomo wa lango.
Deogratius Munishi ‘Dida’ ataendelea kusimama langoni, beki wa kulia Shomary Kapombe, kushoto Oscar Joshua na katikati Kevin Yondan na Nahodha, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Nooij ameanzisha washambuliaji wengi leo kwa sababu anataka Stars ivune mabao mengi katika mchezo huo wa kwanza, ili kurahisisha mchezo wa marudiano. Kwa ujumla, Nooij amerudi kikosi kile kile kilichoifunga 1-0 Zimbabwe katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam Mei 18, isipokuwa tu Nyoni amechukua nafasi ya majeruhi Frank Domayo.
Stars imekuwa na maandalizi mazuri kwa ajili ya mchezo huu, ikianza na kambi ya Botswana karibu wiki mbili na baadaye siku tisa Tukuyu mkoani Mbeya.
Stars iliyofika hatua hii baada ya kuitoa Zimbabwe kwa jumla ya mabao 3-2 ikishinda 1-0 nyumbani na sare ya 2-2 Harare, ikifanikiwa kuitoa Msumbiji itapangwa katika Kundi C ambalo lina timu za Zambia, Cerpe Verde na Niger zilizofuzu moja kwa moja hatua hiyo, kuwania tiketi ya Morocco mwakani.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu hiyo iweze kufuta uteja kwa Mambas.
Stars imekuwa ikinyanyaswa na Msumbiji miaka ya karibuni na mara mbili imewahi kutolewa na Mambas katika hatua za awali za AFCON. Kuwania Fainali za Ghana mwaka 2008, Stars ikiwa chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo ilifungwa 1-0 Dar es Salaam katika mchezo wa mwisho wa kundi.
Kuwania Fainali za mwaka jana Afrika Kusini, Stars ikiwa chini ya kocha Mdenmark, Kim Poulsen, ilitolewa kwa penalti 5-4 na Msumbiji baada ya sare ya jumla ya 2-2. Kila la heri Taifa Stars.
KOCHA Mart Nooij amewaanzisha pamoja washambuliaji Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, Mrisho Ngassa na John Bocco katika mchezo wa kwanza dhidi ya Msumbiji, hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco.
Katika mchezo huo, utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo, Mholanzi huyo amewaanzisha pia viungo Mwinyi Kazimoto katika dimba la chini na Erasto Nyoni juu yake.
Ngassa na Ulimwengu watashambulia pembeni wakati Bocco na Samatta watacheza mbele ya mdomo wa lango.
![]() |
Wakali watatu; Kutoka kulia Mbwana Samatta, Mrisho Ngassa na Thomas Ulimwengu wataanza pamoja na John Bocco chini |
Nooij ameanzisha washambuliaji wengi leo kwa sababu anataka Stars ivune mabao mengi katika mchezo huo wa kwanza, ili kurahisisha mchezo wa marudiano. Kwa ujumla, Nooij amerudi kikosi kile kile kilichoifunga 1-0 Zimbabwe katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam Mei 18, isipokuwa tu Nyoni amechukua nafasi ya majeruhi Frank Domayo.
Stars imekuwa na maandalizi mazuri kwa ajili ya mchezo huu, ikianza na kambi ya Botswana karibu wiki mbili na baadaye siku tisa Tukuyu mkoani Mbeya.
Stars iliyofika hatua hii baada ya kuitoa Zimbabwe kwa jumla ya mabao 3-2 ikishinda 1-0 nyumbani na sare ya 2-2 Harare, ikifanikiwa kuitoa Msumbiji itapangwa katika Kundi C ambalo lina timu za Zambia, Cerpe Verde na Niger zilizofuzu moja kwa moja hatua hiyo, kuwania tiketi ya Morocco mwakani.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu hiyo iweze kufuta uteja kwa Mambas.
Stars imekuwa ikinyanyaswa na Msumbiji miaka ya karibuni na mara mbili imewahi kutolewa na Mambas katika hatua za awali za AFCON. Kuwania Fainali za Ghana mwaka 2008, Stars ikiwa chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo ilifungwa 1-0 Dar es Salaam katika mchezo wa mwisho wa kundi.
Kuwania Fainali za mwaka jana Afrika Kusini, Stars ikiwa chini ya kocha Mdenmark, Kim Poulsen, ilitolewa kwa penalti 5-4 na Msumbiji baada ya sare ya jumla ya 2-2. Kila la heri Taifa Stars.
0 comments:
Post a Comment