MSHAMBULIAJI Wilfried Bony ameonyesha heshima kwa timu yake ya zamani, Swansea City baada ya kuifunga akiichezea timu yake ya sasa, Manchester City, lakini hakushangilia.
Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya England, Bony alitokea benchi kuchukua nafasi ya Muivory Coast mwenzake, Yaya Toure na akafunga bao la nne dakika ya 90 katika ushindi wa 4-2 Uwanja wa Liberty.
Yaya Toure aliifungia City mabao mawili kipindi cha kwanza dakika ya 21 na 74, wakati bao lingine la timu hiyo lilifungwa na James Milner dakika ya 36.
Mabao ya wenyeji yalifungwa na Gylfi Sigurdsson dakika ya 45 na Bafetimbi Gomis dakika ya 64.
Kikosi cha Swansea kilikuwa; Fabianski, Richards, Fernandez, Williams, Taylor, Cork, Shelvey/Britton dk77, Dyer/Barrow dk73, Sigurdsson/Emnes dk83, Montero na Gomis.
Manchester City; Hart, Zabaleta, Demichelis, Mangala, Kolarov, Toure/Bony dk85, Fernandinho/Kompany dk80, Milner, Lampard/Navas dk59, Silva na Aguero.
Bony hakushangilia kuonyesha heshima kwa klabu yake ya zamani, Swansea baada ya kuifungia bao la nne Manchester City leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA


.png)
0 comments:
Post a Comment