Na Mahmoud Zubeiry, RUSTENBURG
TIMU ya taifa ya Zimbabwe imeanza vizuri michuano ya Kombe la COSAFA baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mauritius jioni ya leo katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi A Uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg, Afrika Kusini.
Zimbabwe, moja ya timu zinazopewa nafasi ya kuchukua Kombe mwaka huu, ingeweza kuibuka na ushindi mnono zaidi kama si juhudi za kipa wa Mauritius, Kevin Jean-Louis.
Hatimaye mabao ya Carlos Rusere na Ronald Chitiyo kila kipindi yakatosha kuifanya Zim ianzie kileleni mwa kundi hilo.
Katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo, Namibia ililazimishwa sare ya bila kufungana na vibonde Shelisheli kwenye Uwanua huo huo.
Namibia ilitengeneza nafasi nyingi nzuri za kufunga, lakini wakaishia kukosa mabao ya wazi kutokaa na ubora wa kipa Jose Euphrasie.
Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi za Kundi B Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace, Lesotho, wakianza na Madagascar Saa 11:00 jioni na baadaye, wageni waalikwa kutoka Afrika Mashariki, Tanzania wakimenyana na Swaziland Saa 1:30 usiku, saa moja zaidi kwa saa Tanzania.

![]() |
| Wachezaji wa Zimbabwe wakishangilia bao la kwanza leo |
Namibia ilitengeneza nafasi nyingi nzuri za kufunga, lakini wakaishia kukosa mabao ya wazi kutokaa na ubora wa kipa Jose Euphrasie.
Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi za Kundi B Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace, Lesotho, wakianza na Madagascar Saa 11:00 jioni na baadaye, wageni waalikwa kutoka Afrika Mashariki, Tanzania wakimenyana na Swaziland Saa 1:30 usiku, saa moja zaidi kwa saa Tanzania.

.png)
0 comments:
Post a Comment