BAO pekee la Lionel Messi dakika ya 65 limeipa Barcelona ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Atletico Madrid Uwanja wa Vicente Calderon jioni ya leo katika mchezo wa La Liga.
Kwa ushindi huo dhidi ya timu ya Diego Simeone, Barca sasa inajihakikishia taji la ubingwa wa La Liga, ambalo linakuwa taji la 23 katika historia yao.
Kikosi cha Atletico Madrid kilikuwa; Oblak, Juanfran, Godin, Gimenez, Siqueira, Suarez/Garcia dk68, Gabi, Koke, Turan/Mandzukic dk72, Griezmann na Torres/Niguez dk80.
Barcelona: Bravo, Alves, Alba/Mathieu dk80, Pique, Mascherano, Rakitic/Rafinha dk87, Busquets, Iniesta/Xavi dk82, Messi, Neymar na Pedro.
Lionel Messi akishangilia baada ya kuifungia bao pekee Barcelona bao pekee leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA


.png)
0 comments:
Post a Comment