• HABARI MPYA

    Sunday, May 17, 2015

    MWADUI NA STAND ZAGOMBEA SAINI YA CHANONGO

    Haroun Chanongo anatakiwa na timu zote, Stand United, Mwadui na Toto
    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    WAGENI katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Mwadui FC ya Shinyanga wameanza mazungumzo na winga wa zamani wa Simba SC, Haroun Othman Chanongo kwa ajili ya kumsajili.
    Mwadui iliyopanda Ligi Kuu pamoja na Majimaji ya Songea, African Sports ya Tanga na Toto Africans ya Mwanza inataka huduma za mchezaji huyo ili kuwa na kikosi imara ligi itakapoanza.
    Chanongo ambaye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu amecheza kwa mkopo Stand United ya Shinyanga, pia anatakiwa na timu hiyo pamoja na Toto Africans ya Mwanza.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, Katibu Mkuu wa Mwadui FC, Ramadhani Kilao alisema kwamba wamefanya mazungumzo ya awali na mchezaji huyo, ambayo yamehusu dau la usajili.
    “Tumefanya naye mawasiliano, ametueleza kwa sasa ni majeruhi, lakini ametupa muda ili atoe jibu sahihi juu ya kiasi ambacho anahitaji,” alisema. Kwa upande wake, Chanongo naye amekiri kufanya mazungumzo na Mwadui, huku pia akisema Stand United nayo pia inataka kuendelea naye.
    “Mwadui walinipigia na kunieleza juu ya dhamira yao, kwa sasa sitaweza kujibu lolote hadi hapo nitakapofungua PoP (plasta ngumu).
    Chanongo amefungwa PoP baada ya kuumia mwishoni mwa Ligi Kuu na ana wiki mbili zaidi kabla ya kufungua plasta hilo gumu. 
    Kuumia huko kumemvurugia mipango yake ya kwenda kufanya majaribio TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
    Mwadui pia ipo katika hatua za mwishoni za kuongeza Mkataba na kocha wao Mkuu, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
    Kilao alisema wakimalizana na Julio, wanatarajia wiki ijayo wataanza usajili, wakianzia na kuwaongezea Mikataba nyota waliopandisha timu chini ya kocha Julio.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWADUI NA STAND ZAGOMBEA SAINI YA CHANONGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top