• HABARI MPYA

    Sunday, May 17, 2015

    MENSAH AFUNGIWA MIEZI MINNE KWA KUSAINI TIMU MBILI KWA WAKATI MMOJA

    BEKI wa Ghana, Jonathan Mensah amefungiwa kucheza soka kwa miezi mine baada ya kugundulika amesaini timu mbili katika uhamisho wake kutoka Serie A kwenda Ligue 1 Julai mwaka 2011.
    Kwa mujibu wa hukumu ya Mahakama ya Usuluhishi ya Mchezo (CAS), beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 24 alikutwa na hatia hiyo akihama Udinese ya Italia kwenda Evian TG ya Ufaransa.
    Taarifa nchini Ufaransa zimesema kwamba mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ghana amefungiwa miezi mine, wakati klabu yake ya sasa, imepigwa faini Euro Milioni 1 kwa kumsajili mchezaji huyo kama huru, wakati alikuwa hajamaliza Mkataba Italia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MENSAH AFUNGIWA MIEZI MINNE KWA KUSAINI TIMU MBILI KWA WAKATI MMOJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top