BONDIA Floyd Mayweather Jr leo ameanza rasmi maisha ya siku zaidi ya 90 katika jela mjini Las Vegas kwa kosa la udhalilishaji.
Bondia huyo ambaye hajanonja kipigo tangu aanze ngumi za kulipwa anayeshikilia taji la WBC katika uzito wa Welter, aliwasili jela akipigwa tafu na nyota wa Hip hop 50 Cent, ambaye alisema bondia huyo atakuwa poa tu katika gereza la Clark County Detention Center mjini Nevada.
Mayweather alihukumiwa kifungo Desemba mwaka jana baada ya kukutwa na tuhuma za kumshambulia mpenzi wake wa zamani Josie Harris, mwaka 2010 lakini kifungo chake kilipelekwa mbele ili kumpa fursa ya kumaliza pambano lake na Miguel Cotto, Mei 5, mwaka huu.
Baada ya kumaliza kifungo chake, inafahamika kwamba Mayweather atapambana na mpinzani wake wa muda mrefu, Manny Pacquaio.
Jala: Floyd Maywether akiongozwa na afande kuingia katika gereza la Clark County Detention Center mjini Las Vegas
Wapambe: Mayweather akisindikizwa na askari Karen Winckler na rafiki yake 50 Cent (kushoto kabisa).
Mjelajela: Mayweather akipozi kuipigwa picha jela
Ghetto la mchizi jela: Mayweather atakuwa anaishi humu kwa siku zaidi ya 90.
0 comments:
Post a Comment