• HABARI MPYA

    Saturday, June 02, 2012

    MBABE CHRIS EUBANK AAMUA KUREJEA ULINGONI


    Comeback: Chris Eubank wants to return to the ring
    Kurejea ulingoni: Chris Eubank anataka kurudi ulingoni


    BONDIA Chris Eubank amefufua ndoto zake za kurejea ulingoni, kwa gwiji huyo wa ndondi Uingereza kutaka kupambana na mpinzani wake wa zamani, Nigel Benn.
    Mbabe huyo mwenye umri wa miaka 45, bingwa wa zamani wa WBO katika uzito wa Middle na Super Middle, amesema kwamba angependa kupambana na Benn kama ambavyo mtoto wake wa kiume, anayepigana katika uzito wa Middle,Christopher Jr.
    Eubank alivyosema: 'Nipo katika uzito wa Light-Heavy kwa sasa na nikimuangalia Bernard Hopkins mwenye umri wa miaka 47 kwa sasa, nafikiri, "kama anaweza kufanya hivi, kwa nini nisiweze, kwa isiwe mimi I?"
    'Kurejea gym? Wow. Kupigwa tena, kupigwa kifuani, kuwa tayari kupokea konde usoni, hizo ni ndoto kwangu, nina hamu sana na hilo.
    'Nilikuwa pia nazungumza na Nigel Benn na nilisema: "Wee kijana, tunatakiwa kurudi".
    'Itakuwa babu kubwa kupigana tena, hususan katika kiwango kile kile sawa na mwanangu wa kiume.'
    Alisema: 'Kwanza, ningehitaji sapoti ya watu. Nisingetaka kufanya kuvuruga heshima niliyojijengea katika jamii kama bondia.'


    Let's get it on: Eubank wants a re-match with his old rival Nigel Benn
    Njoo tuzipige tena: Eubank anataka kurudiana na mpinzani wake wa zamani Nigel Benn.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBABE CHRIS EUBANK AAMUA KUREJEA ULINGONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top