KLABU ya Azam FC, imesema kwamba inachezea rungu la Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa kutaka kumsajili kihuni mchezaji wao, brahim Rajab Jeba.
Meneja wa Azam FC, Patrick Kahemele ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, Jeba anatoka kwenye kituo cha kulea vipaji cha
Azam FC na inakumbukwa kilichowakuta Chelsea baada ya kumsajili Gael Kakuta
kinyemela licha ya kwamba, mchezaji huyo hakuwa na mkataba na klabu ya RC Lens ya
Ufaransa lakini FIFA iliwatia hatiani Chelsea na kuwaamuru wailipe Lens
"Tafsiri yake ni kuwa wachezaji waliolelewa kwenye Academy
hata bila mikataba hufungwa na ile klabu ilyomlea ndiyo maana pesa ya TP
Mazembe kwa Samata ilifika Mbagala kwenye kituo kilichomlea,"alisema Kahemele na kuongeza
"Pili kwa kuwa Ibrahimu Jeba, ambaye Azam ilimtoa kwa mkopo
msimu uliopita kwa klabu ya Villa Squad bado ana mkataba na Azam.
"Kitendo cha Simba kufanya naye mazungumzo na kumhamisha
kinyemela ni uvunjifu wa kanuni za soka zilizowekwa na halitofautiani na tukio
la Chelsea kuzungumza na Ashley Cole nje ya wakati wa usajili, tukio
lililoifanya FA wakati huo iwape adhabu Chelsea,"alisema Kahemele.
Simba inataka kumsajili Jeba kama mchezaji wa Villa Squad iliyoshuka daraja Ligi Kuu na tayari ameanza mazoezi ya awali na Wekundu hao wa Msimbazi katika gym.
0 comments:
Post a Comment