• HABARI MPYA

    Saturday, June 02, 2012

    RONALDO AKINYANYAPAA KIBINTI CHA MIAKA 10 KILICHOVAA JEZI YA BARCELONA

    Ronaldo
    NYOTA wa Real Madrid na Ureno, Cristiano Ronaldo amegoma kusaini autograph kwa binti wa umri wa miaka 10, aliyekuwa amevaa jezi ya Barcelona.
    Katika batua iliyochapishwa na gazeti la Record la Ureno Robert Filipe amesema kwamba binti yake aliamua kuvaa jezi ya Barca kwa mazoezi ya timu yake huko Obidos.
    Hata hivyo, mazoezi ya timu yake yakaahirishwa kwa ajili ya maandalizi ya timu ya taifa ya Ureno  kwa Euro 2012, na binti huyo wa umri wa miaka 10, akaamua kuangalia mazoezi na ndipo alipodharauliwa na nyota huyo wa Seleccao.
    "Nilipokwenda kumchukua, hakuwa na furaha kama ambavyo nilivyomtarajia binti mcheshi, lakini iliniuma kwanza," Filipe alisema. "Nilipomuuliza nini kinaendelea, akasema kwa machungu: 'Cristiano hakutaka kunisainia autograph kwa sababu nimevaa jezi ya Barcelona'.
    "Sikujua niseme nini. Hii ni jezi aliyovaa kwa ajili ya kufanya mazoezi na ambayo alinunuliwa na mama yake aliposafiri kwenda Barcelona.ilikuwa ni ishara ya upendo na hakukua na kingine zaidi (kama angeenda Madrid na jezi dhahiri ingekuwa tofauti), na imeishia kumpa machungu mwanwe. Ureno inacheza na Uturuki mechi ya kirafiki usiku wa leo na imepangwa kundi moja na Ujerumani, Denmark na Uholanzi katika fainali za Euro zinazoanza wiki ijayo Poland na Ukraine.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RONALDO AKINYANYAPAA KIBINTI CHA MIAKA 10 KILICHOVAA JEZI YA BARCELONA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top