MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Danny Welbeck ameifungia bao lake la kwanza timu ya taifa ya England, wakati kikosi hicho cha Roy Hodgson kikiibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ubelgiji katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na Euro 2012 kwenye Uwanja wa Wembley.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21, amejiwekea mazingira ya kuanzishwa kwenye mechi ya kwanza ya Euro dhidi ya Ufaransa Jumatatu kwa bao lake hilo tamu kipindi cha kwanza.
0 comments:
Post a Comment