• HABARI MPYA

    Wednesday, April 03, 2013

    BARCA YABANWA NA AKINA BECKHAM, BAYERN YAIPIGA 2-0 JUVE


    DAVID Beckham akitimiza miaka 38, jana ameiongoza PSG kulazimisha sare ya 2-2 na Barcelona kwenye Uwanja wa Parc des Princes katika Robo Fainali ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.  
    Lakini matokeo hayo yanaiweka PSG katika mlango wa kutokea, kwani sasa Barca wanapewa nafasi kubwa ya kusonga mbele wakicheza mechi ya marudiano nyumbani.
    Barcelona ilikuwa mbele kwa bao 1-0 hadi mapumziko lililofungwa na mwanasoka bora wa dunia kutoka sayari nyingine, Lionel Messi dakika ya 38.
    Zlatan Ibrahimovic aliifunga timu yake ya zamani kipindi cha pili (dakika ya 79) akiisawazishia PSG, lakini Xavi akaifungia bao la pili Barca kwa penalti dakika ya 89.
    Huwezi amini, dakika moja baadaye, PSG wakachomoa na safari hii alikuwa ni Matuidi aliyefunga bao hilo dakika ya 90.
    Katika mchezo huo, kikosi cha PSG kilikuwa: Sirigu, Jallet, Alex, Thiago Silva, Maxwell, Beckham/Verratti dk70, Matuidi, Lucas Moura, Pastore/Gameiro dk76, Ibrahimovic na Lavezzi/Menez dk66.

    Barcelona: Valdes, Dani Alves, Pique, Mascherano/Bartra dk84, Jordi Alba, Xavi, Busquets, Iniesta, Sanchez, Messi/Fabregas dk46, Villa/Tello dk81.

    Stars of the show: Messi is tracked by Beckham
    Utaipenda hii: Messi akitafuta mbinu za kumtoka Beckham
    Battle for the ball: Messi holds off the challenge of Beckham
    Safari: Messi sasa anamtoka Beckham
    Going in for the tackle: Beckham brings down Cesc Fabregas
    Amekula: Beckham amemkwatua Cesc Fabregas
    In the book: Beckham is shown a yellow card by Referee Wolfgang Stark
    Njano: Beckham akionyeshwa kadi ya njano na refa Wolfgang Stark
    On target - again: Lionel Messi opened the scoring for Barcelona with a well-struck volley
    Amefunga tena: Lionel Messi akishangilia bao lake la kwanza jana
    Bao la kusawazisha: Zlatan Ibrahimovic akishangilia bao lake la kusawazisha ambalo lililamikiwa kuwa la offsideControversy: Zlatan Ibrahimovic pulled his side level with a goal that seemed to be clearly offside
    Controversy: Zlatan Ibrahimovic pulled his side level with a goal that seemed to be clearly offside
    Controversy: Zlatan Ibrahimovic pulled his side level with a goal that seemed to be clearly offside
    Katika mchezo mwingine, Bayern Munich iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Juventus mjini Munich, shukrani kwao David Alaba na Thomas Muller wafungaji wa mabao hayo.
    Explosive start: David Alaba gave Bayern Munich the lead inside the opening minute
    Hii kali: David Alaba aliifungia bao la kwanza Bayern Munich na hapa ndivyo alivyoshangilia 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BARCA YABANWA NA AKINA BECKHAM, BAYERN YAIPIGA 2-0 JUVE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top