Na Boniface Wambura, IMEWEKWA SEPTEMBA 1, 2013 SAA 6:30 MCHANA
USAILI wa waombaji uteuzi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) unaendelea na unatarajia kukamilika leo (Septemba 1 mwaka huu).
Kamati ya Uchaguzi ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Hamidu Mbwezeleni ilianza usaili juzi (Agosti 30 mwaka huu) ambapo matokeo ya usaili yanatarajiwa kutangazwa keshokutwa (Septemba 3 mwaka huu).
Kati ya Septemba 4 na 6 mwaka huu, Kamati ya Uchaguzi kupitia Sekretarieti ya TFF itawasilisha kwenye Kamati ya Maadili ya TFF mashauri yote ya maadili ili kujadiliwa na kutolewa uamuzi na kamati hiyo.
Vilevile kati ya Septemba 4 na 6 mwaka huu ni kipindi cha kukata rufani kwenye Kamati ya Rufani ya Uchaguzi kwa masuala yasiyo ya maadili. Kwa watakaokata rufani wanatakiwa kuambatanisha na ada ya rufani kwa Katibu Mkuu wa TFF kabla ya saa 10 kamili jioni ya Septemba 6 mwaka huu.

![]() |
Mgombea urais wa TFF, Athumani Nyamlani kulia akiwa na Dioniz Malinzi, kaka wa mpinzani wake, Jamal Malinzi katika uchaguzi huo. Kwa sasa Dioniz ni Mwenyekiti wa BMT na Nyamlani ni Makamu wa kwanza wa Rais wa TFF. Jamal Malinzi ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Kagera (KRFA).