Na Boniface Wambura, IMEWEKWA SEPTEMBA 1, 2013 SAA 6:30 MCHANA
KIUNGO wa Simba, Jonas Mkude ameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemuongeza mchezaji huyo ili kuimarisha sehemu ya kiungo.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeingia kambini tangu Agosti 29 mwaka huu kwenye hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam.
Timu hiyo imefanya mazoezi leo asubuhi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume wakati kesho Jumatatu (Septemba 2 mwaka huu) saa 10 jioni itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mkude alikuwemo kwenye kikosi cha Stars, lakini akaenguliwa baada ya kupoteza namba katika kikosi cha kwanza cha Simba SC, ila sasa baada ya kukomboa nafasi yake na kufanya vizuri, amerejeshwa kikosini.
Katika mechi mbili alizocheza za Ligi Kuu msimu huu, tayari Mkude ana mabao mawili, aliyofunga yote katika mchezo wa kwanza wa ligi hiyo dhidi ya Rhino Rangers mjini Tabora wiki iliyopita, timu hizo zikitoka 2-2.

![]() |
Amerejeshwa; Jonas Mkude ameitwa tena Taifa Stars baada ya kufanya vitu Simba SC |