• HABARI MPYA

    Sunday, September 01, 2013

    WANASOKA WATATU WA TANZANIA KUKIPIGA UJERUMANI, WAOMBEWA ITC DAR WAANZE KAZI ULAYA

    Na Boniface Wambura, IMEWEKWA SEPTEMBA 1, 2013 SAA 6:34 MCHANA
    CHAMA cha Soka Ujerumani (DBU) kimetuma maombi ya Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wawili wa Tanzania ili wajiunge na klabu mbili tofauti za nchini humo.
    Wa Ulaya wanaongezeka; Shomary Kapombe tayari anacheza AS Cannes ya Ufaransa


    Maombi hayo yaliyotumwa kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni kwa ajili ya wachezaji Henry Claud Egito aliyezaliwa Desemba 31, 1984 jijini Dar es Salaam, na Dominic Johnson aliyezaliwa Agosti 14, 1991 jijini Tanga.
    Wachezaji hao wanaombewa ITC kama wachezaji wa ridhaa. Egito anaombewa hati hiyo ili ajiunge na klabu ya FSV Lokomotive Dresden wakati Johnson anatakiwa na klabu na TSV 1967 Schwabbruck.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: WANASOKA WATATU WA TANZANIA KUKIPIGA UJERUMANI, WAOMBEWA ITC DAR WAANZE KAZI ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top