Na Ezekiel Kamwaga, IMEWEKWA SEPTEMBA 1, 2013 SAA 7:12 MCHANA
KIUNGO wa Simba SC, Kiggi Makassy, kesho anatarajiwa kuwaaga mashabiki wa klabu hiyo kwa ajili ya safari ya India kwa matibabu ya goti lake, aliloumia mapema mwaka huu mjini Dodoma akiichezea timu hiyo mchezo wa kirafiki dhidi ya CDA.
Kiggi aliyejiunga na Simba SC msimu uliopita akitokea kwa wapinzani wa jadi, Yanga SC anatarajiwa kuondoka nchini Septemba 9, mwaka huu kwa matibabu hayo na kabla ya mchezo wa kirafiki kati ya Simba SC na Mafunzo, atawapungia mkono mashabiki Uwanja wa Taifa.
Simba SC, inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, baada ya safari ya mikoa ya Tabora na Arusha kwenye mechi mbili za awali za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, imerejea Dar es Salaam kujiandaa na mechi ijayo ya ligi hiyo, dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro Septemba 14, mwaka huu.
Kama sehemu ya maandalizi ya mechi hiyo, kikosi cha Simba kitashuka dimbani katika Uwanja Mkuu wa Taifa siku ya kesho, Jumatatu Septemba 2, kucheza na Mafunzo ya Zanzibar.
Mechi hiyo itatumika pia kutoa nafasi kwa wapenzi na wanachama wa Simba, pamoja na washabiki wa soka kwa ujumla wake, kupata fursa ya kuwaona kwa mara ya kwanza wachezaji wapya watatu wa klabu ambao hawajawahi kuonekana wakicheza jijini Dar es Salaam.
Wachezaji hao ni Henry Joseph Shindika aliyetoka Kongsvinger ya Norway, Gilbert Kaze na Amissi Tambwe waliotoka katika klabu ya Vital’o ya Burundi, ambao hawakutambulishwa katika Tamasha la Simba Day kama ilivyo ada kwa wachezaji wote wapya.
Viingilio katika mechi hiyo, vinatarajiwa kuwa Sh 20,000 kwa VIP A, Sh 10,000 kwa VIP B, Sh 8,000 kwa VIP C na Sh 5,000 kwa mzunguko.

![]() |
Anaagwa kesho; Kiggi Makassy anakwenda India kutibiwa |