• HABARI MPYA

    Wednesday, December 11, 2013

    ZANZIBAR HEROES SASA KUONDOKA LEO NAIROBI BAADA YA ‘MSOTO’

    Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
    SHIRIKISHO la Soka Kenya (FKF), limesema kwamba tatizo la timu ya Zanzibar kukwama kuondoka nchini hapa baada ya kutolewa katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge limetatuliwa na timu hiyo itaondoka leo.
    Zanzibar Heroes walikwama kuondoka kutokana na shirika la ndege lililotakiwa kuwasafirisha kutolipwa fedha zao, lakini Makamu wa Rais wa FKF, Robert Asembo amesema shirika hilo limekubali kuisafirisha timu hiyo.
    Makamu wa Rais wa FKF, Rober Asembo kushoto akizungumza pembeni ya Katibu wa CECAFA, Nicholas Musonye leo mchana

    “Na siyo Zanzibar tu, timu zote zilizokuwa na matatizo kama hayo, yametatuliwa na zote zitafika kwao leo,”alisema Asembo katika Mkutano na Waandishi wa Habari, hoteli ya Hill Pack, Nairobi mchana wa leo.
    Asembo alisema wamiliki wa hoteli na mashirika ya ndege walikuwa wanakaidi agizo la Serikali la Kenya kutakiwa kutoa huduma hizo kwa ahadi ya kulipwa na serikali na kama wasingekaidi tatizo hilo lisingejitokeza.
    Zanzibar iliishia katika hatua ya makundi kwenye CECAFA Challenge ya mwaka huu, baada ya kuzidiwa kete na Kenya na Ethiopia katika Kundi A- na pia ikashindwa kufuzu kwenda Robo Fainali japo katika kapu la timu mbili maalum zilizomaliza na wastani mzuri katika nafasi za tatu katika makundi yote.
    Kocha wa Zanzibar, Salum Bausi kulia akiwa wachezaji wake jana Uwanja wa Nyayo

    Haya ni matokeo mabaya kwa Zanzibar ikilinganishwa na mwaka jana ilipoweza kushika nafasi ya tatu kwa kuifunga Tanzania Bara.      
    Michuano ya 50 ya CECAFA Challenge inafikia tamati kesho Uwanja wa Nyayo kwa mechi mbili, ya kusaka mshindi wa tatu kati ya Zambia na Tanzania na Bara na fainali baina ya wenyeji, Kenya na Sudan.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZANZIBAR HEROES SASA KUONDOKA LEO NAIROBI BAADA YA ‘MSOTO’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top