• HABARI MPYA

    Monday, June 09, 2014

    HATIMAYE CAMEROON WAENDA BRAZIL BAADA YA MZOZO WA POSHO KUINGILIWA KATI NA SERIKALI

    KIKOSI cha Cameroon kilitarajiwa kuondoka jana usiku mjini Younde kuelekea Brazil baada ya kutatuliwa kwa mgogoro wa posho zao.
    Waziri Adoum Garoua alisema jana “Kila mmoja yuko tayari kuondoka Saa 3:30 (usiku wa jana) kwenda Brazil. Kila kitu kimefafanuliwa. Hakuna matatizo zaidi,”.
    Wachezaji wa Simba Wasiofinguka jana waligoma kupanda ndege kwenda  Brazil kwa ajili ya Kombe la Dunia ili kushinikiza malipo ya posho za kushiriki michuano hiyo na kubaki katika hoteli yao mjini Yaounde, wakati Waandishi wa Habari walikuwa nje ya ofisi za Shirikisho la Soka Cameroon kupata maelezo juu ya sakata hilo.
    Ndege ilitarajiwa kuondoka Yaounde Saa 3:00 asubuhi ya jana kwenda Brazil, wakati Cameroon inacheza mechi yake ya ufunguzi Ijumaa na Mexico.
    Yamekwisha: Wachezaji wa Cameroon walitarajiwa kuondoka usiku wa jana kwenda Brazil

    Wachezaji wa Cameroon wiki iliyopita walitaka kugoma hadi kwanza wapewe posh zao, lakini wakasitisha mgomo huo na kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ujerumani Jumapili iliyopita, liliripotia gazeti la L'Equipe la Ufaransa. Cameroon ipo Kundi A na wenyeji Brazil, Croatia na Mexico.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HATIMAYE CAMEROON WAENDA BRAZIL BAADA YA MZOZO WA POSHO KUINGILIWA KATI NA SERIKALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top