MABAO mawili ya Jozy Altidore jana yameipa Marekani ushindi wa 2-1 dhidi ya Nigeria katika mchezo wa mwisho wa kujiandaa na Kombe la Dunia Uwanja wa EverBank Field mjini Jacksonville.
Altidore alimaliza ukame wa mabao ndani ya miezi sita kwa klabu na timu yake ya taifa kwa kufunga bao moja kila kipindi na kuifanya Marekani iende Brazil ikitoka kushinda mechi tatu mfululizo za kirafiki.
Mshambuliaji wa Nigeria, Victor Moses alizima matumaini ya Tim Howard kumaliza mechi bila kufungwa katika mchezo wake wa 100 akiifakia Marekani baada ya bao la dakika za lala walama kwa penalti.



.png)
0 comments:
Post a Comment