• HABARI MPYA

    Wednesday, June 04, 2014

    KIGAGULA GHANA AIBUKA NA KUTAMBA; “MIMI NDIYE NINAYEMLOGA CRISTIANO RONALDO, WATAHANGAIKA SANA KUMTIBU, HAPONI NG’O”

    Na Robin Bairner, ACCRAH
    MGANGA wa kienyeji wa Ghana, Nana Kwaku Bonsam amesema yeye ndiye anayemloga nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo ili asicheze mechi dhidi ya Black Stars katika Kombe la Dunia.
    Mganga huyo amesema Ronaldo atatumia dawa yoyote, lakini hawezi kupona.
    Mshambuliaji huyo wa Real Madrid anasumbuliwa na maumivu ya mishipa fulani laini katika mguu wake na atakosa mechi za nchi yake kujiandaa na Kombe la Dunia dhidi ya Mexico na Ireland na Nana Kwaku Bonsam amesema yeye ndiye anayemuwangia Mwanasoka huyo Bora wa Dunia.
    Namloga Ronaldo; Mganga wa kienyeji wa Ghana, Nana Kwaku Bonsam amesema anamloga mchezaji huyo wa Ureno asicheze Kombe la Dunia

    “Nafahamu kinachomsumbua Cristiano Ronaldo katika maumivu yake, mimi ndiye namsababishia,” amesema kigagula huyo akizungumza na Redio Angel FM ya Ghana. 
    “Niko makini sana juu ya hili. Wiki iliyopita, nilikwenda kutafuta mbwa wanne na nimewapata na kutengeneza uchawi maalum unaitwa ‘Kahwiri Kapam’.
    “Nilisema hivi miezi minne iliyopita, kwamba nitamshughulikia Cristiano Ronaldo na kumfanya asicheze Kombe la Dunia, au angalau akose mechi dhidi ya Ghana na njia pekee ninayoweza kufanya ni kumsababishia maumivu.
    Pole nyota; Cristiano Ronaldo anasumbuliwa na maumivu ya mguu, ambayo kila baada ya muda yanaelezewa tofauti na wataalamu
    Majeruhi haya hayawezi kutibiwa na dawa yoyote, hawawezi kuona kinachomsumbua kwa sababu ni nguvu za kiza. Leo, watasema ni goti lake, kesho mguu, siku nyingine ni kitu kingine pia.”

    Ghana itacheza na Ureno Juni 26 mjini Brasilia, ambao utakuwa mchezo wao wa mwisho wa Kundi G, walilopangwa pamoja na Ujerumani na Marekani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIGAGULA GHANA AIBUKA NA KUTAMBA; “MIMI NDIYE NINAYEMLOGA CRISTIANO RONALDO, WATAHANGAIKA SANA KUMTIBU, HAPONI NG’O” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top