• HABARI MPYA

    Sunday, June 08, 2014

    MSIBA: MZEE SMALL HATUNAYE

    Na Dina Ismail, DAR ES SALAAM
    MWIGIZAJI wa siku nchini, Said Ngamba maarufu kama Mzee Small, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa Rufaa ya Muhimbili mjini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu. 
    Mtoto wa marehemu, Muhiddin amethibitisha taarifa za kifo cha baba yake, ambaye alikuwa anasumbuliwa na shinikizo la damu.
    Muhiddin alisema baba yake alizidiwa jana nyumbani kwake, Tabata, Dar es Salaam na kukimbizwa Muhimbili, ambako umauti ulimfika.

    Mzee Small kushoto akiwa na Bi Chau enzi za uhai wake

    Mzee Small jina lilitokana na ufupi wake, ni miongoni mwa waigizaji wa mwanzoni nchini waliokuwa wamebakia ambao walifungua njia kwa wengine wengi wanaotamba kwa sasa.
    Alipata umaarufu zaidi wakati alipokuwa akiigiza kama mume wa Chausiku Salum ‘Bi Chau’ kuanzia Redioni hadi kwenye Televisheni.
    Kwa kwa miaka miwili sasa, afya ya Mzee Small imekuwa ikisumbua na mara kadhaa alilazwa hospitali na kuruhusiwa baada ya ahueni. Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MSIBA: MZEE SMALL HATUNAYE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top