• HABARI MPYA

    Sunday, June 08, 2014

    TP MAZEMBE WANA KAZI NA ZAMALEK LEO LUBUMBASHI

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    TP Mazembe ya DRC leo itakuwa kwenye Uwanja wake wa Mazembe, Lubumbashi kuikaribisha Zamalek ya Misri katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Mazembe yenye washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu katika mechi zake mbili za kwanza ilifungwa 1-0 na El Hilal ya Sudan na kushinda 1-0 dhidi ya ndugu zao, As Vita ya Kinshasa, DRC. 
    Tegemeo; Mshambuliaji wa TP Mazembe, Thomas Ulimwengu leo atawashughulisha mabeki wa Zamalek
    Mchezo wa leo utakaonza Saa 11:00 kwa saa za Afrika Mashariki ni muhimu Mazembe kushinda ili kufufua matumaini ya kutwaa taji la tano la michuano hiyo.  
    Baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na AS Vita jana, Hilal imefungana kila kitu na timu hiyo ya DRC, pointi nne na wastani sawa wa mabao ya kufunga na kufungwa, kila timu imefunga mabao matatu na kufungwa matatu.
    Mazembe na Zamalek kila moja ina pointi tatu na timu itakayoshinda leo, ndiyo itamaliza mzunguko wa kwanza kileleni, lakini zikitoka sare timu zote zitalingana kwa pointi kwenye Kundi B na kutazamwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.  
    Kundi B nalo linahitimisha mzunguko wa kwanza leo, Esperance ikimenyana na CS Sfaxien, zote za Tunisia na Al Ahly Benghazi ya Libya ikimenyana na ES Setif ya Algeria.
    Sfaxien ina pointi nne sawa na Setif, lakini ipo kileleni kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa. Benghazi ina pointi tatu, wakati Esperance watupu, hawana pointi. 
    Mzunguko wa pili wa Ligi ya Mabingwa unatarajiwa kuanza baada ya Kombe la Dunia Julai.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TP MAZEMBE WANA KAZI NA ZAMALEK LEO LUBUMBASHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top