• HABARI MPYA

    Sunday, July 20, 2014

    JESHI MISRI LAMUONDOA MOHAMED SALAH CHELSEA

    MUSTAKABALI wa Mohamed Salah katika klabu ya Chelsea upo shakani, baada ya kutakiwa kurejea nyumbani kwao, Msiri kuchukua mafunzo ya jeshi.
    Salah, aliyehamia Stamford Bridge kutoka Basle ya Uswisi Januari mwaka huu, ameruhusiwa kuishi England kwa kigezo cha kushiriki masomo.
    Pamoja na hayo, usajili wake umesitishwa na Wizara ya Elimu ya Juu Misri, tovuti ya soika ya www.kingfut.com imesema, maana yake mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anaweza kurudi nchini mwao.

    Jeshini kwanza; Mo Salah anatakiwa kurudi nyumbani kupata mafunzo ya Jeshi

    Ikiwa Salah, aliyeichezea Chelsea mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC Wimbledon jana atatakiwa kurejea nyumbani, hataruhusiwa kuondoka tena Misri hadi akamilishe mafunzo ya kijeshi, yanayochukua mwaka mmoja hadi mitatu.
    "Salah ameelesea namna alivyoshitushwa juu ya uamuzi huu," amesema Mkurugenzi wa timu ya taifa ya Misri, Ahmed Hassan.
    "Ameniambia anajaribu kuiwakilisha Misri katika njia nzuri zinazowezekana. Na haya ndiyo matokeo yake kutoka kwa nchi yake?'
    Kikao kinatarajiwa kufanyika baina ya FA ya Misri, benchi la ufundi la timu ya taifa na Waziri wa Elimu ya Juu, kutafuta suluhisho.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JESHI MISRI LAMUONDOA MOHAMED SALAH CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top