• HABARI MPYA

    Friday, March 20, 2015

    HARRY KANE AULA KIKOSI CHA ENGLAND KWA MARA YA KWANZA

    MSHAMBULIAJI machachari wa klabu ya Tottenham Hotspur, Harry Kane amejumuishwa katika kikosi cha wakubwa cha timu ya taifa ya England kwa mara ya kwanza baada ya kocha wa timu hiyo Roy Hodson kuvutiwa na kiwango chake.
    Kane,21,ambaye amekuwa tegemezi wa kocha Maurcio Pochettino katika kikosi cha Tottenham, tayari ameifungia klabu hiyo magoli 26 katika michuano yote msimu huu. "Nchi nzima imeshangazwa na kiwango cha Harry Kane, anafanya vizuri. Itakuwa ajabu endapo sitomjumuisha katika kikosi changu " alisema kocha Roy Hodson.

    Harry Kane ameitwa katika kikosi cha wakubwa cha timu ya taifa ya England kwa mara ya kwanza baada ya kocha wa timu hiyo Roy Hodson kuvutiwa na kiwango chake

    Kikosi kilichoitwa na Roy Hodson ni makipa; Fraser Forster (Southampton), Joe Hart ( Man City), Mabeki; Gary Cahill Chelsea), Leighton Baines ( Everton), Nathaniel Clyne (Southampton), Phil Jageilka ( Everton)
    Luke Shaw (Man u), Phil Jones (Man u), Chris Smalling (Man u), Kyle Walker (Tottenham) na Kieran Gibbs ( Arsenal).
    Viungo ni; Ross Barkley ( Everton), Michael Carrick ( Man u), Fabian Delph ( Everton), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana ( Liverpool), James Milner (Man City), Theo Walcott ( Arsenal), Andros Townsend (Tottenham) na Raheem Sterling ( Liverpool), wakati washambuliaji ni; Harry Kane ( Tottenham), Danny Welbeck (Arsenal), Daniel Sturridge ( Liverpool) na Wayne Rooney ( Man U).
    Kikosi hicho kitashuka dimbani katika uwanja wa Wembley ijumaa ijayo kuwakaribisha Lithuania ukiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa Ulaya 2016 na siku nne baadaye watasafiri kwenda kucheza mechi ya kirafiki na timu ya taifa ya Italia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HARRY KANE AULA KIKOSI CHA ENGLAND KWA MARA YA KWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top