Kiungo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Salvatory Edward (kushoto) akiwa na Kocha Msaidizi wa timu ya taifa, Taifa Stars, Salum Mayanga kwenye benchi leo wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Salvatory ameombwa kwa muda kumshikia kocha wa makipa wa Taifa Stars, Patrick Mwangata ambaye amekwenda kushiriki kozi ya ukocha. Stars leo imetoka sare ya 1-1 na Malawi.
0 comments:
Post a Comment