‘KIBIBI KIZEE’ cha Turin kimeinuka tena. Habari ndiyo hiyo. Juventus ya Italia imefuzu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kufuatia ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Borussia Dormund usiku huu Uwanja wa Westfalenstadion, Dortmund, Ujerumani.
Juve sasa inakwenda Robo Fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-1, baada ya awali kupata ushindi mwembamba nyumbani wa 2-1.
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Carlos Tevez aliifungia Juve bao la kwanza dakika ya tatu, kabla ya Alvaro Morata kufunga la pili dakika ya 70 kwa pasi ya Muargentina huyo.
Tevez aliyewahi pia kuchezea Manchester City, aliifungia Juve bao la tatu zikiwa zimesalia dakika 10 na hicho kinakuwa kipigo cha nne kwa
Dortmund katika mechi nne walizokutana na Juventus kwenye michuano ya Ulaya.
Timu nyingine zilizotinga Robo Fainali ni PSG, Monaco zote za Ufaransa, Atletico Madrid, Real Madrid, Barcelona, FC Porto na Bayern Munich.
Droo ya Robo Fainali itapangwa Ijumaa Saa 7:00 mchana kwa saa za Afrika Mashariki.
Carlos Tevez akipongezwa na wenzake baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Borussia Dortmund usiku huu
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3001196/Borussia-Dortmund-0-3-Juventus-agg-1-5-Carlos-Tevez-Alvaro-Morata-strikes-secure-Champions-League-quarter-final-spot-Serie-giants.html#ixzz3UmHznJ3w
0 comments:
Post a Comment