• HABARI MPYA

    Friday, March 20, 2015

    TWIGA STARS WAENDA ZAMBIA NA MATUMAINI

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    MSAFARA wa watu 25 wa timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars), umeondoka Alfajiri ya leo kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza dhidi ya timu ya Taifa ya Wanawake ya Zambia siku ya jumapili.
    Kikosi hicho kiliagwa na kukabidhiwa bendera jana mchana katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya safari hiyo.
    Kocha wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage alisema jana baada ya kukabidhiwa bendera kwamba kikosi chke kipo vizuri na ana matumaini ya kwenda kufanya vizuri Zambia.
    “Tumekuwa na maandalizi mazuri kwa muda wa takriban mwezi mzima na vijana wapo vizuri kuelekea mchezo huo.
    Kikosi cha Twiga Stars baada ya kukabidhiwa bendera jana
    Kwa kweli tuna matumaini ya kufanya vizuri,”alisema Kaijage.

    Twiga Stars inaanzia hatua ya pili katika kuwania kufuzu kwa Fainali za Afrika kwa Wanawake baada ya kuwa katika nafasi za juu kwa viwango barani Afrika, na endapo itafanikiwa kuwaondoa Wazambia itafuzu moja kwa moja kwa fainali hizo.
    Msafara huo umengozwa na Blassy Kiondo (Mjumbe wa Kamati ya Utendaji), Beatrice Mgaya (kiongozi msaidizi), Rogasin Kaijage (kocha mkuu), Nasra Juma (kocha msaidizi), Furaha Francis (Meneja), Christine Luambano (Daktari) na Mwanahamis Abdallah (Mtunza vifaa).
    Wachezaji waliokweda Zambia ni Asha Rashid, Mwajuma Abdallah, Mwanahamis Omar, Donisi Minja, Amina Bilal, Fatuma Bashiri, Esther Chabruma, Shelda Mafuru, Maimuna Kaimu, Najiat Abbas, Stumai Abdalla, Fauma Issa, Thereza Yona, Fatuma Hassan, Fatuma Omary, Sophia Mwasikili, Fatuma Khatibu na Etoe Mlenzi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TWIGA STARS WAENDA ZAMBIA NA MATUMAINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top