• HABARI MPYA

    Friday, March 20, 2015

    BEACH SOCCER YAWASILI SALAMA MISRI

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Taifa ya soka la Ufukweni (Beach Soccer) imewasili salama jijini Cairo nchini Misri tayari kwa mchezo wa marudiano dhidi ya wenyeji kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa Afrika zitakazofanyika Visiwa vya Shelisheli.
    Msafara wa timu ya soka la Ufukweni ulipokelewa na maofisa wa Ubalozi wa Tanzania waliopo nchini Misri,  pamoja na viongozi wa chama cha soka nchini Misri (EFA).
    Leo jioni kikosi kinatarajia kufanya mazoezi mepesi, kabla ya kesho kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja utakaofanyika mchezo siku ya jumapili.
    Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri timu ya soka la ufukweni katika mchezo wake wa marudiano siku ya jumapili dhidi ya Misri.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BEACH SOCCER YAWASILI SALAMA MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top