Na Mahmoud Zubeiry, RUSTENBURG
KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooij amemuondoa rasmi kiungo chipukizi, Said Juma ‘Makapu’ katika programu za mchezo wa kesho dhidi ya Lesotho Kombe la COSAFA mjini hapa.
Makapu, ambaye kwao Zanzibar huitwa Kizota akifananishwa na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Said Nassor Mwamba ‘Kizota’ (sasa marehemu) leo alikuwa benchi wakati wenzake wakifanya mazoezi.
Stars imefanya mazoezi yake ya mwisho usiku wa leo Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace kabla ya mchezo wake wa ufunguzi wa Kundi B kesho dhidi ya Swaziland Saa 1:30 usiku, ambao utatanguliwa na mechi nyingine ya kundi hilo kati ya Lesotho na Madagascar itakayoanza Saa 11:00 jioni.
Ni Uwanja huo huo wa Royal Bafokeng Sports Palace uliopo mbali kidogo na katikati ya Jiji la Rustenburg, ambako mechi za Kundi zitafanyika.
Makapu amekuja mjini hapa akiwa majeruhi, baada ya kuumia mgongo katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, akiichezea klabu yake, Yanga SC ikifungwa 1-0 na Ndanda FC mjini Mtwara.
Pamoja na kufurahia mwanzo mzuri katika msimu wake wa kwanza akiiwezesha Yanga SC kutwaa ubingwa, lakini mchezaji huyo tunda la mpango wa maboresho ya timu ya taifa amemaliza ligi kwa machungu ya maumivu ya mgongo.
Kuelekea mchezo wa kesho, Mholanzi Nooij anataka kuendeleza mafanikio yake katika michuano ya COSAFA wakati anafundisha Msumbiji kabla ya kuja Tanzania.
“Hii si mara ya kwanza kwangu kama kocha kushiriki mashindano haya ya COSAFA,” amesema. “Nchi wanachama wa COSAFA zote zina timu madhubuti za taifa, ambayo inafanya michuanno iwe ya ushindani. Hicho ndiyo ambacho tunakitafuta timu ya taifa ya Tanzania,”.

![]() |
| Said Makapu alikuwa benchi tu leo wakati wenzake wanafanya mazoezi |
![]() |
| Wachezaji wa Taifa Stars wakinywa maji baada ya kumaliza mazoezi leo |
![]() |
| Wachezaji wa Taifa Stars wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace leo |
Ni Uwanja huo huo wa Royal Bafokeng Sports Palace uliopo mbali kidogo na katikati ya Jiji la Rustenburg, ambako mechi za Kundi zitafanyika.
Makapu amekuja mjini hapa akiwa majeruhi, baada ya kuumia mgongo katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, akiichezea klabu yake, Yanga SC ikifungwa 1-0 na Ndanda FC mjini Mtwara.
Pamoja na kufurahia mwanzo mzuri katika msimu wake wa kwanza akiiwezesha Yanga SC kutwaa ubingwa, lakini mchezaji huyo tunda la mpango wa maboresho ya timu ya taifa amemaliza ligi kwa machungu ya maumivu ya mgongo.
Kuelekea mchezo wa kesho, Mholanzi Nooij anataka kuendeleza mafanikio yake katika michuano ya COSAFA wakati anafundisha Msumbiji kabla ya kuja Tanzania.
“Hii si mara ya kwanza kwangu kama kocha kushiriki mashindano haya ya COSAFA,” amesema. “Nchi wanachama wa COSAFA zote zina timu madhubuti za taifa, ambayo inafanya michuanno iwe ya ushindani. Hicho ndiyo ambacho tunakitafuta timu ya taifa ya Tanzania,”.

.png)
0 comments:
Post a Comment