Bongo Staz imeipata exclusive kutoka SuperSport, kwamba mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana, Asamoah Gyan ameamua kustaafu soka ya kimataifa.
Mchezaji huyo tegemeo wa Black Stars amewasilisha barua Chama cha Soka Ghana jana usiku, kuwataarifu uamuzi wake , ambao umeungwa mkono kwa kiasi kikubwa na famili yake na rafiki zake.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26, ameichezea Ghana mechi 59 na zaidi anaachana na soka ya kimataifa kutokana na kuzomewa kwa kukosa penalti kwenye Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, Ghana ikitolewa na Zambia, iliyoibuka bingwa baadaye.
Kwa kukumbukia kwamba alikosa penalti pia dhidi ya Uruguay kwenye Robo Fainali ya Kombe la Dunia ambayo kama Ghana wangepata wangeweka historia ya kuwa timu ya kwanza ya Afrika kucheza Nusu Fainali ya Kombe la Dunia uamuzi wake umekuja wakati mwafaka.
Alisema amekuwa akiichezea Ghana tangu ana umri wa miaka 17 mwaka 2003. Kwa sasa mshambuliaji huyo anacheza kwa mkopo Al Ain ya UAE kutoka Sunderland ya England.
Gyan ameifungia Ghana mabao 28 katika mechi 59 tangu acheze mechi ya kwanza dhidi ya Somalia miaka tisa iliyopita.

0 comments:
Post a Comment