![]() |
Chollo |
BEKI wa kulia wa Simba SC, Nassor Masoud ‘Chollo’ atakuwa
nje ya Uwanja kwa wiki sita, kufuatia kuumia kwake katika mazoezi ya timu ya
soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wiki mbili zilizopita timu hiyo ikijiandaa
na mechi na Ivory Coast.
Daktari wa Simba SC, Cossmas Kapinga ameiambia BIN
ZUBEIRY jana kwamba baada ya kufanyiwa vipimo, imebainika Chollo
anatakiwa kuwa nje ya Uwanja kwa wiki sita, jambo ambalo litamfanya akose hadi
michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Kapinga alisema kwamba Chollo ameumia mfupa wa katikati ya
goti, kama walivyoumia beki wa zamani wa Simba, Mganda Joseph Owino ambaye kwa
sasa yupo Azam FC na kiungo wa timu hiyo, Uhuru Suleiman ambao wote
walilazimika kuw anje ya Uwanja wa msimu mzima.
“Tofauti yake Chollo na akina Owino ni kidogo sana, yeye (Chollo)
haujavunjika wote, lakini wenzake ulivunjika wote, pamoja na yote wiki sita ni
nyingi. Anaweza asionekane kanisa uwanjani mwaka huu, kwa sababu hadi apone
aanze taratibu, ni mtihani,”alisema Kapinga.
Kuumia kwa beki huyo si pigo kwa klabu yake tu, bali hata
kwa Taifa Stars, kwani Chollo amekuwa chaguo la kwanza kote huko.
0 comments:
Post a Comment