• HABARI MPYA

    Tuesday, September 03, 2013

    YAMETIMIA, WENGER AMSAINI OZIL KWA DAU LA REKODI ARSENAL NA MSHAHARA KUFURU

    IMEWEKWA SEPTEMBA 3, 2013 7:04 USIKU
    KLABU ya Arsenal imemsaini Mesut Ozil kutoka Real Madrid kwa dau la rekodi katika klabu hiyo, Pauni Milioni 42.5.
    Kiungo huyo amesaini Mkataba wa miaka mitano kwa mshahara wa Pauni 140,000 kwa wiki, baada ya kukamilisha vipimo vya afya nchini Ujerumani Jumatatu, licha ya Paris Saint-Germain kutokea na ofa nzuri mapema siku hiyo ya mwisho ya usajili.
    Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger aliwahi kumtaka kiungo huyo miaka sita iliyopita, lakini Ozil, ambaye atavaa jezi namba 11 Uwanja wa Emirates, sasa ameshawishika kumfuata Mjerumabi mwenzake, Per Mertesacker na Wenger katika klabu hiyo.
    Ozil alisaini Real Madrid kutoka Werder Bremen mwaka 2010 kwa ada ya Pauni Milioni 12.4.
    Star saviour: Ozil has joined Arsenal for a club-record £40million fee
    Nyota ametus: Ozil amejiunga na Arsenal kwa dau la rekodi katika klabu hiyo, Pauni Milioni 42.5
    Stint: Ozil has played 158 times for Real in just over three years
    Anafaa: Ozil amecheza mechi 158 Real katika miaka zaidi ya mitatu
    Fanatic: Arsenal fans show their support for Ozil outside their training ground in Colney
    Fanatic: Arsenal fans show their support for Ozil outside their training ground in London Colney

    WACHEZAJI GHALI WA AWALI ARSENAL

    Santi Cazorla (Malaga, Pauni Milioni 16.5 - Agosti 2012)
    Andrey Arshavin (Zenit, Pauni Milioni 15- Februari 2009)
    Samir Nasri (Marseille, Pauni Milioni 12.5- Julai 2008)
    Sylvain Wiltord (Bordeaux, Pauni Milioni 11 - Agosti 2000)
    Thierry Henry (Juventus, Pauni Milioni 10.5 - Agosti 1999)
    Balancing act: Real are selling Ozil because they have signed other attacking players, including Gareth Bale
    Kata mti, panda jiti: Real imemuuza Ozil kwa sababu imemsaini Gareth Bale kwa dau la rekodi ya dunia
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: YAMETIMIA, WENGER AMSAINI OZIL KWA DAU LA REKODI ARSENAL NA MSHAHARA KUFURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top