• HABARI MPYA

    Monday, June 09, 2014

    BREAKING NEWS; AC MILAN YAMFUKUZA SEEDORF, INZAGHI KOCHA MPYA RASSONERI

    KLABU ya AC Milan imemfukuza kocha Clarence Seedorf na kumteua Filippo Inzaghi kurithi mikoba.
    Mholanzi, Seedorf alianza kazi San Siro mwezi Januari mwaka huu, akirithi mikoba ya Massimiliano Allegri baada ya klabu kuanza vibaya msimu huu, lakini naye ametupiwa virago baada ya Milan kushika nafasi ya nane Serie A.
    Inzaghi, gwiji wa San Siro kama Seedorf, hajawahi kufundisha timu ya wakubwa, lakini amepandishwa kutoka timu ya vijana ya Milan chini ya umri wa miaka 19.
    Kazi basi: Clarence Seedorf amefukuzwa AC Milan
    Hotseat: Inzaghi, pictured during his Milan playing days, has been appointed the new AC Milan manager
    Mtu mpya: Inzaghi, pichani enzi zake akiichezea Milan ameteuliwa kuwa kocha mpya AC Milan 

    Taarifa yao imesema; "AC Milan inapenda kutaarifu kwamba, kocha Clarence Seedorf amefukuzwa, na timu ya kwanza imekabidhiwa kwa Pippo Inzaghi hadi Juni 30, 2016,".
    Kufukuzwa kwa Seedorf, kufuatia Rais wa Milan, Silvio Berlusconi kusema Ijumaa kwamba kiungo huyo wa zamani wa Rossoneri alichangia matokeo mabaya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BREAKING NEWS; AC MILAN YAMFUKUZA SEEDORF, INZAGHI KOCHA MPYA RASSONERI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top